Facebook

Sunday, 18 May 2014

Gerardo Martino ajiuzulu Barcelona !!




 
Gerardo Martino ataacha kazi ya Ukocha wa Barcelona mara baada ya Jana kupokonywa Ubingwa wa La Liga baada kutoka Sare 1-1 na Atletico Madrid ambao wameutwaa Ubingwa huo na kuiacha Barca ikitoka mikono mitupu Masimu huu kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu 2007/08.
Akizungumza mara baada ya Mechi hiyo ya Jana, Martino alisema: “Nasikitika sana tumeshindwa kutimiza malengo yetu ambayo Klabu hii Siku zote imeyaweka na kutimiza!”
Martino alishika wadhifa huo Mwezi Julai Mwaka Jana na kumbadili Tito Vilanova ambae alijiuzulu baada kuugua.
Kazi yake hapo Barcelona ilikuwa ya kwanza kwa Martino, Raia wa Argentina, nje ya Marekani ya Kusini tangu ashike wadifa wa Ukocha wa Miezi 6 huko Tenerife, Spain.
Akiwa na Barca, Martino alisimamia ushindi wa Mechi 40 kati ya 59 lakini wakapokonywa Ubingwa wa La Liga, kutupwa nje ya UCL kwenye Robo Fainali na kufungwa Fainali ya Copa del Rey na Real Madrid.

0 comments:

Post a Comment