Facebook

Wednesday 10 September 2014

Apple wazindua bidhaa mpya.

Kampuni ya Apple imezindua saa ya kisasa -
the Apple Watch - ambayo ni bidhaa yake
mpya tangu iPad ya kwanza na tangu kifo cha
mmoja wa waasisi wake Steve Jobs.
Kifaa hicho huendesha programu tumishi
(apps) na pia hufuatilia mienendo ya kiafya
na vilevile huwasiliana na iPhone.
Wakati wapinzani wa Apple tayari wana saa
za mtindo huo, wataalam wanasema Apple
ina historia ya kuchelewa kuleta bidhaa zake
sokoni lakini hubadili kabisa mwelekeo wake.
Apple pia imezindua simu aina mbili ambazo
ni kubwa kuliko za zamani.
iPhone 6 ina skrini yenye ukubwa wa
sentimita 11.9 na iPhone 6 Plus skrini yake
ina ukubwa wa sentimita 14.0, mabadiliko
ambayo wachambuzi wanasema yatazuia
wateja kuhamia simu za Android.
Apple vilevile imetangaza huduma mpya ya
malipo ijulikanayo kama 'Apple Pay' ambayo
mkurugenzi mkuu Tim Cook amesema ana
imani "itachukua nafasi ya pochi".

0 comments:

Post a Comment