Facebook

Friday 26 September 2014

Inakisiwa kuwa zaidi ya raia 3000 kutoka Ulaya ni wafuasi wa Islamic State

Idadi ya raiya kutoka Uropa wanaojiunga
na kundi la wapiganaji wa Kiislamu nchini
Syria na Iraqi imeongezeka hadi zaidi ya
3,000 kulingana na mkuu wa kitengo cha
kupambana na ugaidi bara la ulaya.
Gilles de Kerchove ameonya kuwa
mashambulizi ya hewa yanayofanywa na nchi
za Magharibi yataongezea hatari ya
mashambulizi ya kulipiza kisasi katika bara la
Ulaya.
Vikosi vikiongozwa na Marekani vimetekeleza
mashambulizi ya hewa mia mbili dhidi ya
wanamgambo wa Islamic state wa Iraqi tangu
Agosti na Jumatatu iliyopita wakaanza kulenga
wale walioko Syria.
Bunge la Uingereza litapiga kura kwa
mashambulizi ya hewa dhidi ya Iraqi siku ya
Ijumaa.
Kundi la IS wameteka sehemu kubwa za Syria
na Iraqi katika miezi ya hivi karibuni.
CIA inakisia kuwa kundi la IS linaweza kuwa na
wapiganaji mpaka 31,000 huko Iraq na Syria,
mara tatu zaidi ya wale waliohofiwa.

Mashambulizi haya yaliotekelezwa siku ya
Alhamisi na ndege za Marekani, Saudi na UAE
zilikuwa zinalenga mitambo 12 ya kusafisha
mafuta nchini Syria .
Msemaji wa Pentagon Rear Admiral John Kirby
alisema kuwa kusudi la mashambulizi haya ya
hewa halikuwa kuwaua wanamgambo hao lakini
ilikuwa kuharibu maeneo ambayo yalikuwa
yakiletea kundi hilo fedha kupitia soko nyeusi.
Baadaye, siku ya Ijumaa, wabunge wa
Uiungereza wataulizwa kuunga mkono
mashabulizi dhidi ya wanamgambo wa IS Iraqi
lakini sio Syria.

Chanzo:BBC

0 comments:

Post a Comment