Facebook

Tuesday 9 September 2014

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi na Boko Haram.

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria,
Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi
wakati wa mapambano na wanamgambo wa
kiislamu Boko Haram.

Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa
siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria
lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa
Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa
ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la
Adamawa.

Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo
amesema kuwa kanali Adeboye
anaendela vizuri.

Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu
ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi
wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo
katika jimbo hilo kufungwa.
Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji
mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa
himaya za kiislamu

0 comments:

Post a Comment