Facebook

Friday 12 September 2014

Miaka 8 jela kwa jaribio la kutaka kumuua mkosoaji wa Rais wa Rwanda

Watu wanne - Watanzania wawili na
Wanyarwanda wawili- waliokutwa na hatia ya
kutaka kumuua mkosoaji wa Rais wa Rwanda
Paul Kagame nchini Afrika Kusini wamehukumiwa
kwenda jela kwa miaka minane kila mmoja. Mkuu
wa zamani wa jeshi la Rwanda Jenerali Faustin
Kayumba Nyamwasa alinusurika jaribio hilo
karibu na nyumbani wake jijini Johannesburg
mwaka 2010. Rwanda imekuwa ikikanusha
kuhusika na tukio hilo. Waendesha mashtaka
awali walitaka adhabu ya miaka kumi na mitano.
Jaji Stanley Mkhari amesema watu hao hawakuwa
wahusika wakuu, bali walikodishwa kufanya
hivyo.

0 comments:

Post a Comment