Facebook

Wednesday 10 September 2014

Wafungwa wapigwa risasi mahakamani Afrika Kusini.

Wafungwa wawili wamepigwa risasi
walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka
katika mahakama moja nchini Afrika
Kusini.
Afisa mmoja kutoka wizara ya sheria aliambia
chama cha wanahabari nchini humo kwamba
wafungwa waliokuwa wanasubiri kusikilizwa
kwa kesi yao waliokota silaha kutoka kwenye
jaa la taka.
Inaarifiwa wafungwa hao walianza kufyatuliana
risasi na maafisa wa polisi.
Tukio hilo lilitokea katika mahakama kuu mtaa
wa Mthatha katika mkoa wa Eastern Cape.
Mthunzi Mhaga, ambaye ni waziri wa sheria,
alisema kuwa mfungwa mmoja alijeruhiwa
mguuni wakati wa ufyatulianaji risasi.
''Walijaribu kutoroka walipoingia ndani ya
majengo ya mahakama , '' alisema bwana
Mhaga.
''Baada ya kuipata bunduki, walianza
kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi, ''
aliongeza kusema bwana Mhaga.
Alisema kuwa polisi waliweza kudhibiti hali.
Kufuatia visa vya hivi karibuni vya ufyatulianaji
risasi mahakamani mjini Pretoria na Cape
Town, waziri wa sheria alisema kuwa
atahakikisha uwepo wa sheria z akudhibiti
ulinzi katika majengo ya mahakama.

0 comments:

Post a Comment