Facebook

Wednesday 10 September 2014

Tahadhari kuhusu gesi za sumu

Mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya anga
la Umoja wa Mataifa Michel Jarraud,
ametoa tahadharti kuwa dunia nzima
inapaswa kushughulikia mabadiliko ya hali
ya anga haraka iwezekanavyo la sivyo
muda unakwisha.
Takwimu mpya kutoka kwa shirika hilo,
zinaonyesha kuwa viwango vipya vya gesi
yenye sumu ya Carbon katika anga ya dunia
viko juu zaidi.
Pia shirika hilo linasema kuwa kiwango cha
gesi ya sumu ya Carbon Dioxide kinaendelea
kuongezeka kwa kasi kuliko hali ilivyokuwa
miaka mitatu iliyopita.
Shrika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO,
linasema kuwa viwango vya gesi chafu
viliongezeka kwa kasi zaidi tangu mwaka 1984.
Bwana Michel Jarraud alisema kuwa hapana
shaka kwamba mabadiliko ya hali ya anga
yanashuhudiwa na kwamba hali inaendelea
kuwa mbaya zaidi.
Umoja wa mataifa unasema kuwa kuongezeka
kwa gesi hizo kunasababisha mabadilko mabaya
ya hali ya hewa hali ambayo inahitaji kuwe
kauli moja ya mkataba wa dunia nzima kuweza
kukabiliana na hali hiyo.

0 comments:

Post a Comment