Facebook

Thursday 11 September 2014

Q Chilla alamba dili nono

Msanii wa muziki wa Bongofleva Abubakari
Katwila almaarufu kama Q Chief amevunja
ukimya kwa kupata dili la mkataba wa
mamilioni na kampuni ambayo itakuwa
ikisimamia kazi zake za muziki
zitakazotengenezwa kwa ubora wa hali ya
juu.

Akiwa menye furaha, Q Chila mwenyewe
ameonekana rasmi katika picha
akikabidhiwa mkataba huo kutoka Qs
Mhonda Company chini ya mmilikiQs
Joseph Mhonda ambaye amesema kuwa
atasaidia kumrudisha Q Chief katika chati
na kumvusha kuelekea mbali zaidi.
Aidha Mhonda ameongea na  na
kusema kuwa katika mkataba huo mkubwa
na Q Chief watazindua bendi itakayokuwa
ikifanya kazi zake na wasanii wenzake
watakaosimamiiwa na kampuni hiyo ya Qs
Mhonda.
Q Chief amesema kuwa kwa takriban miaka
mitano amekuwa kimya katika vyombo vya
habari na anga ya muziki ikiwa ni sehemu
ya kuyapitia maisha mengine nje ya muziki,
ila anamshukuru Mungu kwa kupata
mkataba huo mkubwa wa kumrudisha tena
kwa nguvu zote kwa mashabiki wake.

0 comments:

Post a Comment