Facebook

Wednesday 10 September 2014

Mbwa anayepiga kazi kama binadamu.

Kutana na Lemon, mbwa anayependa kufanya
kazi za nyumbani kama binaadam. Lemon
hupenda kwenda kuchota maji na anaweza
kulima vizuri kwa kutumia jembe la plau.
Mmiliki wake, Alexander Matitsyn alimnunua
Lemon baada ya kustaafu kazi ya jeshi.
Fani yake akiwa katika jeshi la Urusi ilikuwa
kufunza mbwa jinsi ya kutekeleza majukumu
mbalimbali, hivyo si ajabu aliweza
kumfundisha Lemon 'ujanja'.

"Hupenda kujifunza na kujaribu mambo
mapya na huwa hasahau" amesema bwana
Matitsyn.

0 comments:

Post a Comment