Facebook

Friday 12 September 2014

MADEGA "NILIMPITISHA OKWI ACHEZE SIMBA"

Mwenyekiti wa zamani wa Yanga ambaye
yupo kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na
Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Imani Madega
Wilbert Molandi na Julieth Patrick
MWENYEKITI wa zamani wa Yanga ambaye
yupo kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na
Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Imani Madega, amefunguka
juu ya kilichotokea kuhusu kesi ya Yanga na
mchezaji Emmanuel Okwi.
Madega ambaye anajulikana kwa kuwa na
misimamo mikali, amefunguka kuwa
maamuzi yaliyotolewa na kamati yake
ambapo na yeye alikuwemo siku ya hukumu
ya kesi hiyo, ni sahihi na kusisitiza kuwa
hakuna tatizo kisheria kwa Okwi kuichezea
Simba baada ya kuonekana Yanga ilikiuka
mkataba wake na Mganda huyo.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo jana ofisini
kwake, Posta jijini Dar es Salaam, baada ya
kuwepo malalamiko ya chini kwa chini kuwa
aliihujumu Yanga kutokana na kutokuwa na
maelewano mazuri na Mwenyekiti wa Yanga,
Yusuf Manji.
Madega ameliambia gazeti hili kuwa, licha ya
kuwa yeye ni mwanachama halali wa Yanga,
lakini kutokana na dhamana kubwa aliyopewa
katika taifa, aliuweka pembeni uanachama
wake na kufanya kazi aliyopewa katika kutoa
maamuzi sahihi juu ya sakata hilo la Okwi.
Aliongeza kuwa kilichowaponza Yanga ni
barua ya kuvunja mkataba na Okwi
waliyoipeleka TFF na kudai ilirahisisha kazi
kwa kamati kutoa maamuzi hayo ambayo
anayaona ni sahihi na kudai Yanga
walijichanganya wenyewe.
“Mimi nilishangaa Yanga kuandika barua na
kuipeleka TFF kudai eti hawana imani na
mimi kwa kuwa nina kesi na Manji. Najua
wanataka kunigombanisha na wanachama wa
Yanga.
“Sitaki kuzungumzia sana suala hilo kiundani
kwa sababu limeshamalizika na maamuzi
yameshatolewa, kikubwa ni kwamba sitapinga
maamuzi yaliyotolewa na kamati yangu kwa
sababu ni maamuzi sahihi na kila kitu kipo
wazi.
“Niliweka pembeni uanachama wangu wa
Yanga na kufanya kazi niliyopewa kwa
manufaa ya taifa zima, lengo ni kuendeleza
soka nchini.“Ukiisoma barua waliyoandika
kutokuwa na imani na mimi ni wazi ililenga
ugomvi binafsi kati ya Manji na mimi na siyo
klabu, ndiyo maana TFF iliamua kutupilia
mbali pingamizi hilo baada ya kuonekana
hoja zao hazina mashiko.
“Ninaomba kuwaambia Wanayanga wote
kuwa niliondoka Yanga nikiwa sina kinyongo
na ugomvi na mtu yeyote, waelewa na walijue
hilo,” alisema Madega ambaye kitaaluma ni
mwanasheria.

0 comments:

Post a Comment