Facebook

Monday 8 September 2014

MUME ADAI TALAKA BAADA YA KUSHINDWA "MAJUKUMU YA NDOA"

Bwana mmoja jijini Mumbai nchini India,
amepewa talaka yake, baada ya kulalamika
kuwa hawezi kukata "kiu kubwa" aliyokuwa
nayo mke wake ya kufanya tendo la ndoa.
kwa mujibu wa tovuti ya Metro - Mwanaume
huyo akiwa amechoka, alifika katika
mahakama inayoshughulikia masuala ya
kifamilia mwezi Januari, akidai kuwa mke
wake amekuwa akimnyanyasa kwa kutaka
kufanya tendo la ndoa, tangu walipofunga
ndoa mwaka 2012, na kuwa amekuwa
akitumia 'mabavu na udikteta' wakati akitaka
jambo lake.
Na hakuishia hapo: bwana huyo ameiambia
mahakama kuwa mke wake pia alithubutu
hata kumpa dawa za kuongeza nguvu, na
kutishia 'kutembea' na wanaume wengine
kama atashindwa kukata kiu yake kubwa.
Mume huyo akiwa taabani- ambaye amesema
amesumbuliwa na maradhi ya kidole tumbo
'appendicitis' kutokana na kutopumzika,
alipewa talaka aliyokuwa akidai.
"Kwa kuwa mshtakiwa (mke) hakutokea
mahakamani, ushahidi wa mshtaki (mume)
haujapingwa. Na hivyo mahakama hii haina
budi, ila kukubali ushahidi uliowasilisha"
amesema Jaji Laxmi Rao.

0 comments:

Post a Comment