Facebook

Friday 12 September 2014

Clouds kulishitaki gazeti la Aman kwa kumchafua Diva.

Kampuni ya Clouds Media Group yenye makao makuu jijini Dar Es Salaam inataka kulishitaki gazeti la Aman kwa kumchafua mmoja wa watangazaji wake mahiri Loveness Malinzi alimaarufu kama "Diva Loveness";mtoto wa Rais wa Shirikisho la Soka Nchini "TFF" Jamal Malinzi.

Diva huwa anatangaza kipindi cha "Ala za Roho" nyakati za usiku na yeye mwenyewe ameshaweka wazi kutoka kimapenzi na msanii Crazy G.K ambaye yuko masomoni hivi sasa katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kuputia mitandao ya kijamii hususan instagram.

Clouds Media Group kupitia ukurasa wao wa Facebook;Jahazi Clouds FM waliandiki hiki ......

Jahazi Clouds FM
Kutokana na Kichwa cha habari kwenye gazeti
la AMANI la tarehe 11/09/2014 kilichosema:
DIVA: ZITTO NI MUME WANGU. Adai ni mke
anayetambulika kisheria. Habari iliyoandikwa
na Shakoor Jongo.
Sisi kama Clouds Media Group tunathibiisha
kuwa Loveness Malinzi (DIVA) hakuwahi
kuhojiwa na mwandishi yeyote wa habari
kutoka gazeti la AMANI wala chombo
chochote cha habari.
Mbali na habari hiyo kumchafua DIVA
ambaye ni mwajiriwa wa Clouds Media , pia
imemchafua Mheshimiwa ZITTO KABWE na
Clouds Media Group kwa ujumla.
Tunachukua nafasi hii kuutatarifu umma wa
watanzania kuwa taarifa hizo ni za uzushi na
tutachukua hatua za kisheria kwa gazeti hilo
na kwa yeyote aliyehusika kusambaza uzushi
huo.
Kwa upande wa DIVA, anaomba radhi kwa
yeyote aliye athirika na habari hii,
Mheshimiwa ZITTO pamoja na umma wa
watanzania wote.

Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata habari za ukweli na uhakika.

0 comments:

Post a Comment