Facebook

Saturday 6 September 2014

Dr. Harryson Mwakyembe atoa tamko kuhusiana na ajali ya jana Musoma.

Jana September 5 2014 kwenye eneo la
Sabasaba Musoma ilitokea ajali mbaya
sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na
kulihusisha gari jingine dogo ambapo
majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39
Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa
taarifa mpya za vifo zilizotoka muda mfupi
uliopita.

Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi
Dr. Harryson Mwakyembe ilibidi aahirishe
ratiba zake nyingine na kulazimika kwenda
Musoma kuwatembelea majeruhi leo asubuhi
kwenye hospitali ya mkoa pamoja na kwenda
kwenye eneo la ajali kutazama.

Baada ya hapo Waziri Mwakyembe alaongea yafuatayo

‘Inabidi niwape pole Watanzania wote ambao
wamepoteza ndugu jamaa na marafiki, taarifa
za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye
bunge maalum ikawa sasa nitafikaje haraka
Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo
asubuhi kuja hapa’

Kuhusu Wasanii wa bongofleva na waandaaji wa tamasha la Fiesta kufanya maamuzi ya kuahirisha
tamasha ambalo lilikua lifanyike jana
Musoma, Waziri Mwakyembe

hii imenifurahisha sana… inaonyesha Utanzania
Q
hivyo na ninawapongeza sana Clouds Radio
kwa kuguswa na maswala ya jamii’

‘Ajali sasa hivi Tanzania zimechukua nafasi ya
yale magonjwa tunayoyaogopa hasa kwa
kuchukua maisha ya watu na kujeruhi na
kuiingizia serikali gharama kubwa ya
matibabu, hatuwezi kuliangalia hili swala
hivihivi mimi kama Waziri wa uchukuzi
nimewaambia wenzangu kuanzia sasa
Watanzania wataona mabadiliko makubwa’

MATAMKO ALITOYATOA DK.MWAKYEMBE
1. Tunaanza na hawa waliopata ajali,
nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika
Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza…
kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi
ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na
usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa
tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo,
nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa
lakini ni watu tu wameamua, dereva wa
huku anamuona mwenzake na kusema mimi
lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe

2. Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa
madereva wao wote na tunahitaji picha zao
lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi,
hatutaki mabasi ya kupeleka abiria
yaendeshwe na watu tu kwa majaribio,
nataka ushahidi wa kila dereva kwamba
amejiunga na hii mifuko ya akiba ya
Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa
Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’

3. Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo
gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari
ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii
kuhusu binadamu…. bila comprehensive
haendeshi mtu gari kuchukua abiria.

Tamasha la Fiesta lililokua lifanyike Ijumaa
hapa Musoma sasa imefahamika litafanyika
Jumapili ya kesho September 7 2014
ambapo pia imehamasishwa kwa wingi watu
kujitokeza ili mapato hayo yapelekwe kwa
ndugu waliopoteza watu na majeruhi ajalini.

Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata taarifa mbalimbali kwa muda na wakati muafaka.

0 comments:

Post a Comment