Facebook

Wednesday 24 September 2014

Mmiliki wa Kampuni ya ALIBABA ndiye anaeongoza kwa utajiri nchini China.

Mwanzilishi wa mtandao wa Alibaba ndiye
tajiri mkubwa zaidi nchini Uchina kulingana
na rekodi za kampuni yake.
Hili imethibitishwa na ripoti rasmi ya kifedha
ya Hurun.
Bw.Ma ameongoza orodha ya watu tajiri zaidi
nchini Uchina kwa mali ya takriban dola bilioni
25 akifuatwa na mwenyekiti wa Wanda Group
Wang Jianlin.
Matajiri watano katika ya kumi walio katika
orodha hiyo, wanamiliki kampuni za
mitandaoni huku wakiwabwaga wale
wanaomiliki mali isiyohamishika ambao kwa
muda mrefu wamekuwa wakiongoza orodha
hiyo.
Orodha hiyo inahusisha pia kiongozi wa
Tencent Pony Ma.
Mabwenyenye wengine walio katika orodha
hiyo ni mwanzilishi mwenza wa mtandao wa
intanet marufu sana nchini China Baidu, Robin
Li na pia mwanzilishi wa soko la mtandao la
JD.com, Richard Liu Qiangdong.
Bw Liu ambaye kampuni yake ilihusika katika
ubadilishanaji wa hisa huko New York hapo
Agosti mwaka huu, aliorodheshwa katika nafasi
ya kumi.

Kulingana na mtafiti mkuu ambaye pia ndiye
mwenyekiti wa Hurun Report, Rupert
Hoogewerf amesema orodha hiyo imeonyesha
kwamba ari ya kufanya biashara kati ya
wananchi wa Uchina bado haijafa.
"Jack Ma ambaye ameorodheshwa wa kwanza,
ni wa kumi na moja kuwahi kushikilia nafasi
hiyo katika muda wa miaka 16. Hii inaonyesha
mabadiliko makubwa katika uchumi wa Uchina
na kutukumbusha uwezo ulio na masoko
mapya yanayojitokeza kwa sasa.”
Orodha ya matajiri inayotolewa na Hurun
Report ndiyo inayoaminika sana kwa kuwa
hukadiria vizuri utajiri nchini Uchina.

0 comments:

Post a Comment