Facebook

Monday 22 September 2014

Wimbo ''Happy'' wa Pharrel Williams wasababisha matatizo makubwa Iran.

Kikundi cha mashabiki wa muziki
nchini Iran walioiga wimbo maarufu
wa mwanamuziki maarufu wa Marekani
Pharrell Williams, 'Happy'
wamejipata matatni baada ya
kukamatwa na polisi.
Kanda ya video waliyoirekodi
wakiiga wimbo huo, inaonyesha
vijana watatu na wanawake kadhaa
ambao hawakuwa wamejitanda
mitandoa, wakicheza densi kwenye
barabara za nchi hiyo na kwenye paa
za nyumba mjini Tehran.

Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia,
alisema kuwa kanda ya video
inayoonyesha vijana hao wakicheza,
imekiuka maadili ya jamii.
Kituo cha televisheni ya serikali
kilionyesha vijana hao wakikiri
makosa siku ya Jumanne.
Inaarifiwa maelfu ya wananchi wa
Iran wamekamatwa katika miaka 35
iliyopita wakisherehekea na
kujiburudisha kwa mambo ambayo
serikali inaona kama ya kukiuka
maadili.
Hata hivyo vijana hao wanaosema ni
waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa
kushiriki katika kanda hiyo na watu
waliokuwa wanatafuta waigizaji
wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.

Wamekiuka maadili'
Kulingana na taarifa ambazo bado
hazijathibitishwa, watu 13
walikamatwa kuhusiana na kanda
hiyo, ingawa idadi kamili ya
waliokamatwa haijatangazwa rasmi.
Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la
Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu
ambao umekuwa maaruufu sana
duniani, alielezea kukasirishwa na
hatua ya vijana hao kukamatwa.

"Yani siamini kama watoto hawa
walikamatwa kwa kujaribu kueneza
furaha,'' alisema Pharrell katika
ukurasa wake wa Facebook.

Chini ya sheria za kiisilamu,
sharti mwanamke ajitande kutoka
kichwani hadi katika viganja vya
mguu.
Polisi ambao jukumu lao ni
kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi
inafuatwa, hushika doria mara kwa
mara katika barabara za mji mkuu
Tehran.

Kanda hiyo ya "Happy we are from
Tehran" ilionekana kwenye mtandao
wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia
sasa imetazamwa mara 40,000.
Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli
serikali ya Iran wakisema kuwa Iran
ni nchi ambako ni hatia kwa mtu
kuwa na furaha.

Wimbo halisi wa Pharrell 'Happy'
umepelekea maelfu ya watu kote
duniani kuiga video ya wimbo huo na
kutengeza video zao wenyewe. Kutoka
Kenya, Marekani , Uingereza yaani
nchi nyingi duniani tu, watu
wameiga video hiyo kwa kutengeza
yao wenyewe.

Hukumu iliyotolewa
Watu sita nchini Iran waliokamatwa
baada ya kuonekana kwenye kanda ya
video iliyokuwa inaiga wimbo wa
'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri
Pharrel Williams, wamehukumiwa
kifungo cha hadi mwaka mmoja jela
kila mmoja pamoja na adhabu ya
kuchapwa mijeledi 91.

Wakili wa sita hao amesema kuwa
hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi
sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu
jela ikiwa watarejelea kosa hilo.
Kanda hiyo inaonyesha wanaume
watatu na wanawake watatu ambao
hawajafunika vichwa vyao wakicheza
densi kwenye barabara na katika paa
za nyumba mjini Tehran.

Kanda hiyo iliyowekwa kwenye
mtandao wa kijamii wa You Tube,
imetazamwa na zaidi ya watu milioni
moja. Wengi wa waliohusika
kuitengeza kanda hiyo, walifungwa
kwa miezi sita , huku mmoja wao
akifungwa kwa mwaka mmoja,
alinukuliwa akisema wakili wao
Farshid Rofugaran.
Mmoja wa watu waliokamatwa kwa
kucheza densi
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are
from Tehran" ilifikishwa kwa
maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei
baada ya kutazamwa na watu 150,000
kwenye You Tube.

Waliohusika pia walikamatwa na
kushitakiwa kwa kosa la kukiuka
sheria za kiisilamu ambazo
zinawazuia wanaume kucheza densi na
wanawake na pia wanawake kutoka nje
bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye
televisheni wakijitetea kwamba wao
ni waigizaji walihadaiwa kushiriki
katika kanda hiyo Kukamatwa kwa
vijana hao kulizia ghadhabu kutoka
anga za kimataifa huku watetezi wa
haki za binadamu
wakianzisha kampeni kwenye mitandao
ya kijamii kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Paharrel Williams
mwenyewe, ambaye wimbo wake huo,
uliteuliwa kwa tuzo la Oscar,pia
alieleza kukerwa na kukamatwa kwa
watu hao.

Chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment