Facebook

Tuesday 23 September 2014

Marekani imeanza mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la ISIS huko Syria.

Marekani imepanua
operesheni yake dhidi ya
kundi la Dola la Kiislamu
nchini Syria, ikisaidiwa na
mataifa matano ya Kiarabu -
Bahrain, Qatar, Saudi Arabia,
Jordan na Umoja wa Falme
za Kiarabu.

Shirika la uangalizi wa haki
za binaadamu nchini Syria
lenye makao yake mjini
London limesema
mashambulizi hayo yalilenga
mkoa wa kaskazini wa Raqq
na pia mji mkuu wake.
Ukanda wa video
uliyowekwa mtandaoni leo,
unaonesha mabomu
yakidondoka katika eneo la
wazi, miripuko
inayosemekana kutokana na
mashambulizi ya washirika.

Msimulizi katika ukanda huo
anasikika akisema
unaonyesha mashambulizi
kwenye kijiji cha Kfar Derian,
huku akitamka Allah Akbar,
yaani Mungu mkubwa.
Wanaharakati wamesema
mashambulizi hayo yalilenga
maeneo ndani na nje ya mji
wa Raqqa nchini Syria, na
kuongeza kuwa
yalisababisha maafa
miongoni mwa wapiganaji
wa Dola la Kiislamu. Mji wa
Raqqa ndiyo uliyotangazwa
na kundi hilo la wapiganaji
kuwa mji mkuu wao nchini
Syria.

Mwanaharakati
mwigine alieko mkoa wa
kaskazini wa Idlib,
alithibitisha kuwa
makombora kadhaa
yaliushambulia mji wa Kfar
Derian katika saa za asubuhi
leo Jumanne. Mashambulizi
yore yaliwalenga wapiganaji
wa IS pamoja na wale kundi
lenye mafungamano na
mtandao wa Al-Qaeda la Al-
Nusra Front.

Syria yasema iliarifiwa
Ndege za Marekani pia
zilifanya mashambulizi 30
katika mkoa wa Deir al-Zour
mashariki mwa Syria,
unaopakana na Iraq. Serikali
ya Syria ilisema iliafiriwa
mapema juu ya
mashambulizi ya Marekani.
Shirika la habari la Syria,
likiinuku wizara ya mambo
ya nje ya nchi hiyo, limesmea
kuwa upande wa Marekani
ulimuarifu balozi wa
kudumu wa Syria katika
Umoja wa Mataifa mjini New
York kwamba kungefanyika
mashambulizi dhidi ya Dola
ya Kiislamu mkoani Al-
Raqqa.

Uamuzi wa kufanya
mashambulizi ulichukuliwa
mapema siku ya Jumatatu na
kamandi kuu ya Marekani
kwa idhini ya rais Baracl
Obama. Mashambulizi hayo
ndiyo yalikuwa ya kwanza
dhidi ya Dola ya Kiislamu
nchini Syria. Marekani
ilishafanya mashambulizi
dhidi ya kundi hilo nchini
Iraq, lakini ilisema
ingelifuata ndani ya Syria
ikibidi.

Maafisa wa Marekani
walisema mashambulizi hayo
yalianza saa tisa Alfajiri, na
yalifanywa na Marekani,
Bahrain, Qatar, Saudi Arabia,
Jordan na Umoja wa Falme
za Kiarabu. Mkuu wa
upinzani unaoungw amkono
na mataifa ya magharibi
Hadi Bahra, alikaribisha
kuanza kwa mashambulizi
nchini Syria. Viongozi wa
kijeshi wamesema theluthi
mbili ya wapiaganaji
wanaokadiriwa kufikia
31,000 wako nchini Syria,
lakini baadhi ya maafisa
wameelezea wasiwasi kuwa
mashambulizi hayo
yanaweza kumsaidia rais
Assad ,kwa sababu hao
wanapigana kwa sehemu
kumn'goa yeye.

Ufaransa yasema
itamkomboa raia wake
Wakati huo huo, Ufaransa
imesema kuchukuliwa
mateka kwa raia wake nchini
Afghanistan hakutaizuwia
nchi hiyo kushiriki
operesheni za muungano wa
mataifa zinazoongozwa na
Marekani dhidi ya Dola ya
Kiislamu, waziri wa mambo
ya kigeni wa Ufaransa,
Laurent Fabius amewambia
waandishi wa habari.
"Nia ya Ufaransa inaendelea
kuwa ile ile: Tuna mpango
wa kufanya kadiri
tuwezavyo kuwaokoa
mateka, na hasa mateka
huyo lakini kundi moja la
kigaidi haliwezi kushawishi
msimamo wa Ufaransa,"
alisema waziri Fabius.

Raia huyo wa Ufaransa
alitekwa mashariki mwa
Algeria siku ya Jumapili, na
watekaji wake walitoa
mkanda wa video wakitishia
kumuuwa ikiwa Ufaransa
haitasitisha uingiliaji wake
kijeshi nchini Iraq inakounga
mkono operesheni ya
Marekani dhidi ya IS

Chanzo:DW

0 comments:

Post a Comment