Facebook

Tuesday 9 September 2014

Diamond ajitolea kuwasomesha watoto.

Baada ya kupata mafaniko mazuri kupitia muzik.Nyota wa Muziki wa kizazi kipya nchini Nassib Abdul "Diamond Platnumz"
Kupitia matamasha mbalimbali aliyokuwa anayafanya hususan tamasha alilolifanya kipindi cha Krismasi.

Aliendesha Tamasha lijulikanalo kama "Ngolongolo".

Na aliwapata washindi wawili ambao aliwaahidi kuwasomesha;na kweli leo hii ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapeleka shule bora na ya kisasa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Diamond ameandika hiki.

Diamond Platnumz
"Kama unakumbukumbu nzuri wakati nafanya
tamasha langu la Christmass na Ngololo niliuliza
mtoto atakae cheza vizuri Ngololo na kushinda
nimpe zawadi gani?...na wengi walisema
Nimuendeleze kielimu.... Hawa ndio washindi
wetu walioshinda siku ile, ambao siku ya leo
niliwapeleka Rasmi katika Shule ya East Africa
International School iliyopo Mikocheni Dar es
salaam ili waanze Masomo yao...Niliona ni
vyema kama mtoto yupo shule ya kawaida
nimuhamishe international school ili niweze
kumsaidia elimu bora zaidi...Niushkuru pia
uongozi Mzima na wanafunzi wa Shule ya East
Africa International School kwa kuwapokea vizuri"

Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata habari za kina na uhakika.

0 comments:

Post a Comment