Facebook

Tuesday 9 September 2014

Danny Welbeck aing'arisha Uingereza.

Danny Welbeck straika mpya wa Arsenal
alifunga mara mbili kuisaidia England
kuifunga Switzerland kwa bao 2-0 katika
mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2016.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester
United aliziona vyavu dakika ya 58 na lingine
katika muda wa nyongeza. Kwa ushindi huo
England sasa inaongoza kundi E ikiwa na
pointi 3.
Danny alifanya yake baada ya kupewa nafasi
kama straika wa kati akichukua nafasi ya
Daniel Sturridge aliye majeruhi.

0 comments:

Post a Comment