Facebook

Monday 8 September 2014

MAJESHI YATUHUMIWA KUBAKA SOMALIA

Shirika la kutetea haki za binaadam la Human
Rights Watch, limetuhumu majeshi ya Umoja wa
Afrika yaliyopo Somalia kwa kubaka wanawake
na wasichana, na pia kudai ngono ili kuwapa
chakua cha misaada. Taarifa iliyoandikwa
kutokana na ushuhuda uliotolewa na wanawake
na wasichana ishirini na mmoja, imesema baadhi
ya wanajeshi kutoka Burundi na Uganda
walitumia ahadi ya kuwapa misaada ya
kibinaadam ili kuwashawishi wanawake na
wasichana kufanya nao tendo la ndoa. Human
Rights Watch imesema wanawake walinyanyaswa
kijinsia wakati wakitafuta huduma za afya au
maji katika kambi za Umoja wa Afrika. AU
imesema itachunguza tuhuma hizo. Wanajeshi
wapatao elfu ishirini na mbili kutoka mataifa
kadhaa yamekuwa yakipambana na al-Shabaab
nchini Somalia kwa miaka saba iliyopita.

0 comments:

Post a Comment