Facebook

Saturday 13 September 2014

Familia ya Msichana aliyepigwa risasi na Pistorius,Steenkamp yapinga uamuzi wa mahakama.

Familia ya Reeva Steenkamp ambaye
aliuawa kwa kupigwa risasi na
mwanariadha wa Afrika kusini Oscar
Pistorius imekasirishwa na uamuzi wa jaji
wa kesi hiyo baada ya kumpata na hatia ya
mauaji ya kutokusudia na kumuondoalea
mashtaka ya mauaji.

June Steenkamp amesema kuwa mwanawe
ambaye alikufa vibaya hakufanyiwa haki.
Amesema kuwa hakuamini kwamba jaji wa kesi
hiyo alikubali ushahidi wa Oscar Pistorius
kwamba alidhani bi Reeva Steenkamp alikuwa
mtu ambaye alikuwa amevamia nyumba yao.
Hatahivyo mjombaake Pistorius alimshukuru
jaji huyo kwa kumuondolea mashtaka ya
mauaji mwanariadha huyo.
Oscar Pistorius ataendelea kuwa nje kwa
dhamana hadi hukumu yake itakapotolewa
mnamo mwezi ujao.

0 comments:

Post a Comment