Facebook

Thursday 11 September 2014

Florentino Perez "SWEETY DADDY";Roho ya Florentino Perez ilivyomuingia Ed Woodward.


Florentino Perez, Rais wa klabu tajiri duniani ya Real Madrid a.k.a Sweety Daddy, Tycoon katika ulimwengu wa soka.

Mashabiki wa Real Madrid kuanzia viunga vyote vya mji wa Madrid, bara la Ulaya mpaka Asia, Africa kupitia bahari ya Pasific mpaka Marekani ya kusini , Visiwa vya Comoro na viunga vyake, popote pale penye mashabiki wa Real Madrid {Madridista} muda wote wanatabasamu sababu ya "Sweety Daddy", Florentino Perez Perez ;mfanya biashara, mwana siasa na pia amesomea Uhandisi "Civil Engineer", safari yake ya kuwa Rais wa Real Madrid ilianza 1995 ambapo alipoteza kwa Ramón Mendoza kwa kura 700.
 
         Ramón Mendoza {18 Aprili 1927-4 Aprili 2oo1}

Mwaka 2000 ulikua ni wa neema kwake na kwa Madridista, sera alizopoteza nazo kwa Ramón Mendoza miaka mitano iliyopita alizirudia zile zile "Financial status and Management" lakini safari hii aliongeza na ahadi ya kumchukua Luis Figo kutoka kwa wapinzan wao Fc Barcelona, ilionekana kama kituko lakini ni kweli, alipopata urais akatimiza ahadi yake.
 
Akamleta Figo,akaenda kwa "Bibi Kizee wa Turin"Juventus kabeba zao lao la zaman Zidane kwa €75m, Ronaldo, Bekham,Oweni, Robinho,Roberto Carlos na wengine wengi.Galactos ikaanza kukamilika
 
Lakini pia alifanya maamuzi magumu kwa kuwaondoa Fernando Hierro , Fernando Morientes,Steve McManaman,Claude Makélélé.
 
Makélélé kwa kipindi hicho alikuwa kiungo mkabaji bora kabisa duniani (world class) lakini haya ni maneno ya Perez baada ya Claude kuondoka 

 "We will not miss Makélélé. His technique is average, he lacks the speed and skill to take the ball past opponents, and 90% of his distribution either goes backwards or sideways."

Baada ya hilo tukio akaingia tena sokoni,akamchukua Michael Owen, Júlio Baptista, Robinho wote ni washambuliaji hawa sio
viungo na uwezo wao wa kulinda ni mdogo sana.

Perez akamgeukia Patrick Vieira wakashindwana kwenye mshahara tu.Perez aliinua uchumi wa Real Madrid kwa kiasi kikubwa sana kama alivyo ahidi, wachezaji wote bora ilikua halali yake, mwaka 2006 alijiuzulu akidai klabu inahitaji uongozi mpya mwaka 2009 akarudi tena kugombea bahati nzuri hakupata mpinzani kwani alikua mshiriki pekee alieweza kutoa €57,389,000 kama dhamana/ada iliyohitajika,kuanzia hapo akawa Rais, akaendeleza sera zake zile zile na ubabe wake katika soko la usajili,kumbuka huwa hana mbwembwe na maneno mengi pale anapomtaka mchezaji kutoka katika klabu yoyote ile.
 
kwanini usimpende?
kila klabu inatamani kuwa na mtu kama huyu,Alipofanikiwa kuwa Rais mwaka 2009 alianza na Ricardo Kaka kutoka AC Milan akiwa katika ubora wake huku Manchester United wakimchukia kwa dhahama aliyowaletea San Siro wakati mvua inanyesha,Perez akamgekia Cristiano Ronaldo akiwa katika ubora wake,ilikuwa roho ya Sir Alex Ferguson kipindi hicho alifanya kila anachokitaka katika utatu mtakatifu aliokuwa nao kipindi hicho,Carlos Tevez,Cristian Ronaldo,Wayne Rooney ulikuwa unachinjwa Old Trafford kwa namana yoyote ile mpaka ikafikia hatua wapinzani wakawa wanahisi anawahonga marefa,Ronaldo ilikuwa roho ya Manchester United kwa kipindi hicho lakini Perez alitaka kuithibitishia dunia kwamba yeye ni "Sweety Daddy"alienda Manchester na kumvuta Ronaldo kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi duniani Paundi Milionoi 80; akamchukua Karim Benzema katika ubora wake, kisha akaenda kwa majogoo wa Jiji la Liverpool akamchukua Alonso katika ubora wake ,Álvaro Arbeloa katika ubora wake,hauishia hapo "Sweety Daddy akapepesa macho kumtafuta kocha atakayekuweza kuleta ladha na kuwaweka pamoja Galactos  yeye akiwa jukwaani anapata glasi yenye mvinyo akamfuata Mourinho aliyekuwa amechukua Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na Italia akiwa maInter Milan na kisha akamtimua Manuel Pellegrini ambaye alijiunga na Malaga.Sweety Daddy akaendeleza ubabe akawachukua Di maria,Ozil,Khedira.

Sweety Daddy alitaka kuendeleza ubabae wake duniani katika soko la usajili,huku Manchester United,Manchester City,Chelsea na vilabu vingine vikimtolea macho Gareth Bale lakini hawakumpata,kama hiyo haitoshi kocha wa Tottenham wa kipindi hicho alitangaza kabisa hawezi kumuuza Bale kwa pesa yoyote ile itakayoletwa,lakini kwa dunia ya leo hakuna klabu itakayoletewa Paundi Million 100 ikashindwa kumuuza mchezaji,Sweety Daddy akashuka London hana maneno mengi akamchukua mchezaji bora wa EPL na Mchezaji bora chipukizi wa EPL,Gareth Bale akapelekwa Bernabeu akakabidhiwa Jezi namba 11 akiwa amepishana na Mesut Ozil mlangoni akielekea Arsenal

Vivyo hivyo hadi James Rodriguez aliyefanya vizuri sana katika michuano ya kombe la dunia na Toni kross Kama;alivyo waondoa kina Makelele enzi zile, safari hii kaondoka Angel Di maria katika ubora wake binafsi naamini ni miongoni mwa wachezaji 3 bora katika klabu ya Real Madrid msimu uliopita,ilifikia hatua Cristian Ronaldo alikuwa anataka kumuumiza Di Maria mazoezini ili asifuzu vipimo vya afya katika klabu itakayotaka kumsajili,Ronaldo alifanya kila njia kuhakikisha Di Maria anabaki lakini hakuna mwenye sauti mbele ya Sweety Daddy.Mnachester United wakapeleka ofa Sweety Daddy kampandisha ndege Di Maria na kumkabidhi Van Gaal kwa kitita cha Paundi milioni 57.

Baada ya Angel Di Maria kuondoka mambo mengi yalizuka,lakini ni yaleyale tu ulikuwa ni ubabe wa Sweety Daddy
Soma hapa BARUA YA ANGEL DI MARIA KWA MADRIDISTA NA SWEETY DADDY

Aliondoka Mesut Ozil katika dirisha la usajili msimu uliopita kama alivyoondoka Makelele kisha akajiunga Arsenal kwa Paundi milioni 40 lakini wengi waliongea katika sakata zima la kuuzwa kwa Mesut Ozil, Sweety Daddy hakutetereka Madrid ikachukua Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Florentino Perez a.k.a Sweety Daddy ni kiongozi shupavu asiyetetereka katika misimamo yake angekua ndiyo Mkurugenzi wa usajili Pale Old Trafford, Rooney angeshaondoka tangu mwaka 2011,kina Fleacher, Carrick wasingevuka 2010, wangeondoka mapema,Fellain,Young,Valencia wangejua tu kuna timu inaitwa Manchester United wasingeweza kuingia kwenye "dressing room" ya Manchester United hata siku moja.

Smalling,Evance,Cleverley wengine wenye uwezo wa kawaida wangekua Crystal Palace,Burnley,Norwich,Aston Villa huko sasa hivi,Anderson angekua anachoma mahindi kwao Brazil sasa hivi. 

JICHO LANGU LA TATU KWA FLORENTINO PEREZ "SWEETY DADDY" NA EDWARD GARETH WOOD
 
Natamani siku moja kupata kiongozi kama huyu "Sweety Daddy", Edward Gareth Wood naona kwa mbaali anaelekea huko.Hizi ni sababu tatu zinazonifanya niamini hilo...........................

1. Kuhusu hali ya Kiuchumi "Financial Status",Manchester United inashika nafasi ya kwanza kwani imeingia mikataba na makampuni makubwa duniani.Kama ulipata wasaa wa kusikiliza hotuba ya Ed Woodward hapo jana alizungumzia kuhusu faida kubwa inayoipata Manchester United hivi sasa hususan baada ya kuingia mkataba wa kihistoria sio tu katika soka bali katika nyanja yote ya michezo duniaani,hakuna klabu iliyowahi kupata dili nono la udhamini kama la Chevrolet kwa Manchester United,hakuna klabu iliyopata dili nono la utengenezaji wa jezi kama la Addidas hapo 2015 United itapata jumla ya Paundi Million 750 katika dili hilo,Ed Woodward hakuishia hapo alisema bado kuna makampuni mengine yamewasilisha ofa kwa ajili ya kuidhamini klabu hiyo.Kuna wadhamini kama Air Asia amabo wanadhamini safari za Manchester United,AON,DHL,AEROFLOT,EPSON,APEROL Spritz,STC,SINGHA,BWIN,CASILLERO del DIABLO,BULOVA,TOSHIBA,NISSIN,YANMAR haya ni baadhi tu ya makampuni yanayoidhamini Manchester United,usishangae kwa nini Falcao,Van Persie,Rooney wanalipwa mishahara minono inayoonekana ni kufuru kwa klabu nyingine.Usishangae kwa nini Ed Woodward anajeuri ya kutamka kumchukua mchezaji yeyote Van Gaal atakayemuhitaji

kufikia hapa, Kazi alioifanya Perez miaka 5 ndani ya Real Madrid Ed Woodward kaifuta ndani ya miezi 12 kwani ni mtaalamu sana kwenye masuala ya biashara na kikubwa ninachokiona akipata uzoefu mkubwa kwenye masula ya soka hususan usajili atafanya makubwa sana.

Tumeona biashara aliyoifanya dirisha la usajili lililofungwa mwezi uliopita,Manchester United ilichanua makucha yake na kumvuta Ander Herrera kipindi cha kombe la dunia,Kombe la dunia lilipomalizika tu beki mahiri wa Luke Shaw akavutwa kwa pesa iliyoweka rekodi.

Mashabiki ya Manchester United wakiwa na shauku ya kuona wachezaji wenye hadhi ya dunia katika klabu yao Roho ya Florentino Perez "Sweety Daddy" ghafla ikamuingia na Ed Woodward wakavunja benki wakamchukua Angel Di Maria,wakiwa kwenye sherehe ya ujio wa Malaika wakaletewa mchezaji mnyumbulifu mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani,alikuwa muhimili wa Van Gaal kipindi cha fainali za kombe la dunia katika kikosi cha uholanzi,ikumbukwe huyu ndiye mchezaji wa Uholanzi msimu uliopita katika ligi ya Eridivise,anaitwa Daley Blind na kukabithiwa jezi namba 17.

Roho ya Sweety Daddy kupenda vizuri na vilivyobora ikazidi kumuingia,huku kukiwa na "bifu" la chinichini kati ya wakala anayemiliki wachezaji nyota duniani,Jorge Mendez na Sweety Daddy baada ya sakata ya Di Maria,Ed Woodward akatumia mwanya huohuo kumleta mshambuliaji anaeogopewa na mabeki duniani ambaye yuko chini ya Mendez,ni miongoni mwa washambuliaji bora kabisa duniani,nadhani hilo halina ubishi,waulize Chelsea katika fainali ya UEFA SUPER CUP watakueleza kilichowakuta,aliwafanya mabeki kila alichokuwa anakitaka.
Kamuulize Diego Simeone kwa nini almtoa Diego Costa kwa mkopo na kumrudisha baada ya Falcao kutimkia Monaco.
Baada ya kuingiwa na Roho ya Sweety Daddy;Ed Woodward aliweza kumleta Falcao katika dakika za mwisho za usajili huku akizipiku Madrid,Manchester City,ChelseaArsenal na Liverpool katika kudhihirisha kwamba yeye ni Sweety Daddy mpya wa Old Trafford 
 
2. Amejitahidi kurekebisha uongozi wa klabu hususan katika jopo la makocha akishirikiana na Luis Van Gaal kwa kuleta watu wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya "Scouting" n.k
 
3 Aliahidi hakuna jina kubwa lolote atakaloshindwa kulileta Old Trafford, apewe muda klabu isimame kwanza ( Pending hilo) huyu ndiye Sweety Daddy wa Carrington ambaye anaonekana kuingiliwa na Roho Ya Florentino Perez.

Ed Woodward "Tunaweza kufanya vitu ambavyo hakuna klabu yoyote ile inayoweza kuvifanya," 

Nukuu ya pili 
" HUENDA MWAKANI TUKAMRUDISHA KIJANA WETU"

 Roho ya Sweety Daddy imemuingia vilivyo Ed Woodard baada ya kumuondoa Welbeck na kumpeleka kwa mahasimu wao wakubwa Arsenal huku The Gunners wakiwa wamepata mtu ambaye ataleta ladha katika mfumo wa Arsene Wenger,Sweety Daddy namba mbili hana wasiwasi na hilo ameshatoa vitisho na kuahidi kufanya atakavyo katika soko la usajili.

Tayari ameshamhakikishi Luis Van Gaal kumleta nyota yeyote atakayemtaka,huku shabaha kubwa ya Van Gaal ni kuleta Kevin Strootman "Box To Box Midfielder" na kuhamisha kile alichokuwa anakitaka kukifanya Kombe la Dunia kabla ya kuumia kwa Strootman,ikumbukwe Uholazni ilijengwa kupitia kiungo huyu,Strootman ndiyo ilikuwa silaha kuu ya Van Gaal kabla ya kuumia. 
Huku Kevin Strootman akiwa ameshabadili wakala wake na kuhamia kampuni ya mawakala inayomiliki Van Persie ambayo ilifanikisha mipango Van Persie kujiunga United.
 Mashabiki Manchester United taratibu wanaanza kuingiwa na imani kama za Madridista kupitia Sweety Daddy mpya Ed Woodward ambaye amepanga kufanya kila anachotaka katika soko la usajili huku akiwa na sera zilezile zinazofanana na Sweety Daddy "Finacial Status" tumeona tayari klabu imepata mikataba minono na kisajili wachezaji bora na mahiri duniani.
 
Roho ya Florentino Perez imeanza kumuingia vyema Ed Woodward.Tusubiri katika dirisha dogo la Usajili mwezi January tuone ma-Sweety Daddy {Ed Woodward na Florentino Perez} watakapothihirisha ubora wao katika "Finacial Status"

NAWASILISHA HOJA 

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kusoma makala mbalimbali zilizoandikwa kwa kufuata weledi katika uandishi.

Imeandaliwa na.............
                                         Katemi Methsela

0 comments:

Post a Comment