Facebook

Friday 12 September 2014

Mahakama:Pistorius hakukusudia kuua

Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji
inayomkabili Oscar Pistorius, amesema
upande wa mashitaka umekosa
kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la
kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia
kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa
amepinga ushahidi wa upande wa utetezi
kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda
uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva.
Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini
amekana kumuua kwa maksudi , akisema
alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia
nyumba yake.
Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius
alimuua Reeva kwa maksudi,baada ya wapenzi
hao wawili kutofautiana.
Mandishi mmoja anasema kuwa jaji Thokozile
Masipa heunda akachukua hadi Ijumaa
kumaliza uamuzi wake.
Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa
mashahidi waliotoa ushaidi wao katika kesi
hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa
atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua
mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya
wapendanao ya Valentine mwaka jana.
Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa
Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe
Reeva baaya ya ugomvi baina yao lakini
amejitetea akisema alimpiga risasi kimakosa
akidhani mwizi amevamia nyumba yake.

0 comments:

Post a Comment