Facebook

Tuesday 9 September 2014

Majambazi 'wamsulubu' mwalimu Kenya

Mwalimu wa kanisa Katoliki, Magharibi ya
Kenya alijikuta taabani baada ya kutekwa
nyara na majambazi waliomtesa pamoja na
kumpiga msumari kwenye mti msituni,
umbali wa kilomita miambili kutoka
nyumbani kwake.
Peter Asutsa alikaa msituni kwa saa 16 mkono
wake ukiwa unaning'inia kwenye mti kabla ya
kuokolewa na polisi.

Inaarifiwa Peter alipigwa msumari kwenye
kwenye mkono wake mmoja baada ya
majambazi hao kukosa kumpata na pesa zaidi
walizokuwa wakitaka.

Inaarifiwa Asutsa aliizima simu yake na
kuificha ndani ya nguo zake za ndani ambapo
majambazi hao wasingeweza kuipata.
Baada ya majambazi hao kumtelekeza,
alimpigia simu mkewe ambaye aliwaarifu polisi
waliokuja kumuokoa.
Masaibu ya Asutsa yalianza pale alipokwenda
dukani kumnunulia mkewe mgonjwa dawa
katika duka la dawa mjini Kitale Magharibi ya
Kenya.

Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari
alimokuwa anasafiria Asutsa aliamrisha dereva
kusimamisha gari. Kisha akawafungia ndani
akiwa na abiria wengine wawili.

Alitekwa nyara na majambazi waliofika katika
sehemu hiyo kwa gari jingine na kumuingiza
ndani ya gari hilo na hapo ndipo alipogundua
kuwa alikuwa ametekwa nyara.
Walimpora dola 24 na kumtaka asalimu simu
yake , lakini akataa.
Baadaye walimpeleka ndani ya msitu na
kumpigia msumari mtini kupitia kwenye mkono
wake mmoja na kumuacha ndani ya msitu wa
Kaptagat.
Alilazimika kuwatisha na kuwafukuza Fisi na
Mbweha waliokuwa wakitishia kumvamia usiku.
Alisema kuwa alihisi maumivu makali.

0 comments:

Post a Comment