Facebook

Friday 12 September 2014

Mahakama yazuia unywaji Pombe India.


Mahakama ya rufaa nchini India imezuia
mpango wa jimbo la Kerala Kusini mwa
nchi hiyo kupiga marufuku pombe.

Mamia ya wamiliki wa baa walikuwa
wamepinga marufuku hiyo ambayo ingeanza
kutekelezwa Ijumaa hii kwa kusema kuwa
itaporomosha utalii.
Hoteli za kifahari zingeponea marufuku hiyo na
mahakama iliamua kuwa marufuku hiyo haina
msingi.
Jimbo la Kerala ndilo lenye kiwango kikubwa
zaidi cha walevi nchini India.
Uamuzi wa mwisho kuhusu swala hilo,
utatolewa na mahakama kuu.

0 comments:

Post a Comment