Facebook

Monday, 8 September 2014

Taarifa rasmi kutoka kwa Jeshi la Magereza Nchini kuhusu uvumi uliozagaa kuachiwa huru kwa Babu Seya na Mwanae.

Baada ya kuenea kwa taarifa za Babu Seya na Mwanae kuachiwa huru hii ndio taarifa rasmi kutoka kwa Jeshi la Magereza nchini.

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa
kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na
mitandao ya kijamii zikihusisha
kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili
wanaotumikia Kifungo cha Maisha
gerezani.

Wafungwa hao wanaotajwa ni
Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu
Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa
jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa
Watanzania kuwa taarifa hizo zote
zilizotolewa kupitia njia hizo ni za
Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga
kuipotosha jamii kwani wafungwa hao
wapo gerezani na wanaendelea
kutumikia adhabu ya kifungo cha
Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo
kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo
na linawataka wale wote wanaotumiwa
ujumbe wa aina hiyo waepuke
kuusambaza ujumbe huo kwa wengine
bali waufute, kwani kuendelea
kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na
uchunguzi wa kina ili kuwabaini
wanaosambaza ujumbe huo
likishirikiana na Vyombo vingine
muhimu kwa lengo la kuwakamata
wahalifu hao ili mkondo wa Sheria
uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.

BantuTz tuliipata ujumbe ulioambatana taarifa hii lakini haukuwa na uthibitisho wa aina yoyote ile,hatukuweza kukuletea taarifa hiyi,kwani BantuTz tunakuletea habari za uhakika na tuko makini kwa kufuata weledi wa kuandaa habari.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata habari za uhakika.

Imeandaliwa na...
                              Katemi Methsela

0 comments:

Post a Comment