Facebook

Tuesday 9 September 2014

Imedhibitika ile ndege ya Air Malaysia-MH 17 iliyoanguka Ukraine ilidunguliwa.

Wachunguzi wa Kijerumani dhidi ya ndege
ya abiria ya Malaysia ambayo ilipata ajali
huko Ukraine mwezi July na kuripuka
angani wanaeleza kuwa ndege hiyo baada ya
kukumbwa na kitu chenye ncha na
kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye
mionzi mikali ndio chanzo cha ajali.

Mwandishi wa mmoja amesema kwamba ushahidi
huo ni wawazi na kwamba ndege hiyo
ilishambuliwa kwa kombora..

katika ripoti yao
ya kwanza ya kiuchunguzi ,maafisi wa
kijerumani katika masuala ya usalama wa anga
wameeleza kua hakukuwa na tatizo la kiufundi
lililosababisha ndege hiyo ipate ajali, ama
makosa ya rubani yalosababisha ndege aina ya
MH17 kuripuka.

Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba
kisanduku cha kurikodia mwenendo wa ndege
hiyo hakikuonesha kwamba kulikua na dharura.
Abiria wote miambili na tisini na nane
walipoteza uhai pindi ilipo anza safari kutoka
uwanja wa ndege wa Amsterdam kueleke Kuala
Lumpur.kutokana na ajali hiyo kuna shaka
kwamba vikundi vya waasi wa Urusi
viliiidungua ndege hiyo.Lakini mpaka sasa
Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na
ajali hiyo.
Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege
hiyo MH17 inaweza kupatikana pindi mwakani.

0 comments:

Post a Comment