Facebook

Friday 12 September 2014

"Mungu wa Kihindi" awekwa kwenye vitambulisho India.

Maafisa wa utawala nchini India,
wanachunguza ambavyo kitambulisho cha
elektroniki kimetengezwa kikiwa na picha
ya Hanuman mungu wa kihindi na
kutumwa kwa njia ya posta.

Kitambulisho hicho kina picha ya mtu
anayejulikana kama Hanuman kutoka kwa
kipindi kilichojuolikana kama Ramayana, akiwa
amevalia mikufu ya dhahabu na taji la kifalme.

Kitambulisho chenyewe kilipatikana wakati
mfanyakazi wa posta alijaribu kukifikisha kwa
mtu aliyetumiwa ila hangeweza kupata anwani
ya mtu yeyote anayejulikana kama Hanuman.

Alipoangalia kwa picha , aligundua kuwa
huenda ilikuwa mchezo wa danganya toto.
Bado haijaulikana ni nani aliyeweka alama ya
kidole kwenye kitambulisho hicho.

Hanuman alijulikana kama mtoto wa mungu wa
kihindi aliyejulikana kama Pawan, na
kitambulisho chenyewe kina namba ya simu na
anwani ya sehemumoja katika jimbo la
Rajasthan.

Kwa kawaida Hanuman huonekana akiwa na
uso wa Nyani pamoja na mkia. Kuna hekaya za
kale kuhusu Hanuman kote nchini India.
Mfanyakazi huyo wa posta Heeralal Saini,
alikirejesha kitambulisho hicho kwenye kituo
cha posta baada ya kukosa kumpata mtu kwa
jina la Hanuman.

'Hanuman ni nani?'
Hanuman ni mmoja wa miungu wanaobudiwa
na watu nchini India na pia kuna hekaya nyingi
tu kwenye vitabu vya kihindi kumhusu.
Huonekana kama binadamu mwenye uso wa
Nyani na mkia mrefu.

Mara kwa Mara yeye husemekana kuwa mtoto
wa mungu mwingine wa kihindi Pawan na
anasifika kwa kuwa mtiifu na mwaminifu
pamoja na kuwa na nguvu za ajabu.

0 comments:

Post a Comment