Facebook

Monday 8 September 2014

Mwanamke agongwa na Gari la mizigo,Mwili wagawanyika katikati Tanki Bovu-Dar Es Salaam

Taarifa tulioipata hivi punde BantuTz kutoka Mbezi,Jijini Dar es Salaam.

Ajali mbaya imetokea maeneo ya Mbezi,Tanki Bovu baada ya Gari kubwa ya mizigo iliyokuwa inatoka Tegeta na kuelekea katikati ya Jiji la Dar Es Salaam imemgonga mwanamke mmoja ambaye jina lake halikutambulika.

Mwanamke huyo aliyekuwa anavuka barabara aligongwa vibaya na Gari hiyo baada ya kugongwa sehemu ya kiuno na kupelelea kugawanyika kwa mwili wake katikati hali ambayo ilisababisha majonzi na huzuni kwa wananchi walioshuhudia ajali hiyo.

Chanzo cha habari hiyo ni mwendokasi wa gari hilo la mizigo hali iliyopelekwa mwanamke huyo kutojua cha kufanya alipokuwa katikati ya barabara.Aligongwa na gari hilo na moja kwa moja kwenda kutumbukia mtaroni na kufariki papo hapo huku mwili wake ukiwa umegswanyika katikati,huku gari hilo nalo lilipoteza uelekeo na kutumbukia mtaroni

Ajali zinazidi kuikumba nchi yetu,huku maeneo mbalimbali kumeripotiwa ajali mbali ni jukumu la vyombo husika kuchukua hatua madhubuti kuthibiti tatizo hili.

Imeandaliwa na.....
                              Katemi Methsela.

0 comments:

Post a Comment