Facebook

Thursday 11 September 2014

Mtanzania ateuliwa kuwa makamu mkuu wa Rais wa BET Networks.

 

BET Networks, ambayo ipo chini ya kampuni ya Viacom Inc. imetangaza kumwajiri Kay Madati kama makamu mkuu wa rais (Executive Vice President) na pia kama Chief Digital Officer.

Madati, raia wa Tanzania aliyeishi katika nchi nyingi Afrika,
Uingereza na Marekani, ataziongoza timu za BET zinazohusika na masuala yote ya digital, mitandao ya kijamii na pia kusimamia utendaji,uzalishaji wa vipindi, uendelezaji wa teknolojia na bidhaa ndani ya mfumo wa mitandao ya BET Networks.


Madati, ambaye uteuzi wake ulitangazwa wiki iliyopita,atasimamia BET Digital, sehemu ya ushirikishwaji ya BET Networks ambazo kazi zake hufanywa kupitia BET.com, ambayo hujumuisha burudani, muziki, utamaduni na habari. 


BET Mobile, ambayo hutoa apps, ringtones, games na video content kwa vifaa vya wireless; Centric,tv, mtandao ambao ni
nyumbani kwa Centric cable channel;na BET Video On Demand (one of the largest VOD services providing African-American content).


Kabla ya kuchukuliwa na BET, Madati alikuwa Mkuu wa Burudani na Vyombo vya habari katika kitengo cha Global Marketing Solutions cha Facebook Inc.


“His team helped position Facebook Inc. as a key strategic partner for digital and social solutions with film studios, TV networks and
entertainment companies,”
umeandika mtandao wa Forbes.


Kabla ya kujiunga Facebook mwaka 2011, Madati alikuwa akifanya kazi kama ‘Vice President of Audience Experience’ wa CNN Worldwide, ambapo alisaidia kuunganisha vipindi vya kila siku vya CNN katika mitandao ya kijamii.


BET Networks is a global brand,with a trendsetting audience, and
an unrivaled leadership position in the digital and social space. I am excited and energized to unlock more ways for our audience to watch, share, stream, download, and fully engage with all of the
network’s award-winning content,”
alisema Madati


We are in the midst of an unprecedented shift in consumer content consumption and media habits, and I am honored to join BET at a time when we are well poised to redefine digital, mobile,and social TV experiences.”
 
Madati atakuwa chini ya Debra L. Lee, mwenyekiti mtendaji wa BET Networks na makazi yake yatakuwa jijini Los Angeles-Marekani.


“Our audience fully embraces technology and lives on multiple
screens,”
“We are thrilled to welcome Kay to the team, and look forward to his expertise and strategic leadership in the fast-paced world of digital and social media, as consumers continue to turn to BET to discover what’s hot and what’s next.” 
Lee alisema kwenye maelezo yake.

Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata habari mbalimbali kutoka kila pande ya dunia kwa wakati na muda muafaka.

Imeandaliwa na..........
                                      Katemi Methsela.

0 comments:

Post a Comment