Facebook

Tuesday 9 September 2014

MWALIMU ALIYEPIGILIWA KWENYE MTI AZUNGUMZIA MASAIBU YAKE

Mwalimu mmoja nchini Kenya, ambaye aliibiwa
fedha zake na yeye mwenyewe kupigiliwa
msumari kwenye mti, amezungumzia mkasa huo.
Wezi hao walimuibia dola ishirini na nne Peter
Asutsa Alhamisi iliyopita, kabla ya kuupigilia kwa
msumari mkono wake kwenye mti katika msitu
mmoja uliopo Eldoret, magharibi mwa Kenya.
Mwalimu huyo wa mafunzo ya Jumapili (Sunday
School) alikaa kwa saa kumi na sita akiwa katika
maumivu makali kabla ya kuokolewa na polisi.
Amesema aliweza kuwasiliana na mke wake kwa
kutumia simu yake aliyokuwa ameificha kwenye
nguo yake ya ndani.

0 comments:

Post a Comment