Facebook

Monday 8 September 2014

Nyama ya Kiboko yawaletea maafa Afrika Kusini

Watu kumi walikanyagwa na gari lililokuwa
linakwenda kwa mwendo wa kasi
walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau
kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni
mwa wiki.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily
Nation.
Kiboko huyo alikuwa amegongwa na gari na
kufariki Jumamosi jioni katika mkoa wa
Limpopo wakati ambapo wanakijiji walikimbia
katika sehemu hiyo angalau kujipatia kipande
cha nyama.

Msemaji wa polisi aliambia shirika la habari la
AFP kwamba "mnyama huyo aligongwa na
wanakijiji wakaona fursa ya nyama ya bure
ambapo walikimbia kuinyakua na kuanza
kuikatakata''
"Hapo ndipo gari lililokuwa linakwenda kwa
kasi liliwagonga watu 8 walipokuwa wanakata
nyama hiyo na kuwaua,'' aliongeza kusema
msemaji huyo wa polisi.
Watu wengine wawili walifariki kutokana na
majereha yao mabaya wakiwa wanapokea
matibabu hospitalini.
Polisi wanasema kuwa watu wengine saba
akiwemo dereva wa gari hilo wanapokea
matibabu hospitalini.

Imeandaliwa na..
                             Katemi Methsela.

0 comments:

Post a Comment