Facebook

Tuesday 9 September 2014

MIFUPA YA DINOSARIA "GODZILLA" YAPATIKANA TANZANIA

Aina mpya ya dinosaria imetambuliwa
kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini
Tanzania. Mabaki hayo ya dinosaria
yaliyopewa jina la - Rukwatitan Bisepultus -
yalipatikana katika korongo moja kwenye
eneo la Rukwa, kusini magharibi mwa nchi
hiyo. Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa
akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka
mia moja iliyopita, na alikuwa na uzito sawa
na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya
mbele yenye urefu wa mita mbili. Mnyama
huyo ni aina ya titanosaurus -- ambao ni
wakubwa, na wanaokula nyasi. Mabaki ya
wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana
katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara
ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi
cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya
chaki iliumbika) takriban miaka milioni mia
moja na arobaini iliyopita.

0 comments:

Post a Comment