Facebook

Monday 8 September 2014

MZOZO WA NIGERIA NA FIFA WAISHA

Mabingwa wa Afrika, Nigeria huenda
wameepuka kufungiwa kimataifa kuhusiana
na mzozo wa uongozi katika chama cha soka
cha nchi hiyo. Mzozo huo sasa
umesuluhishwa, baada ya Chris Giwa
kuondoa madai kuwa yeye ndio rais wa
shirikisho la sola la Nigeria NFF. Fifa iliipa
Nigeria hadi Jumatatu kupata muafaka. Iwapo
Nigeria ingefungiwa, ingekosa mechi ya
kufuzu Kombe la Mataifa siku ya Jumatato
nchini Afrika Kusini. Shirikisho la soka la
Afrika, Caf lilisema wiki iliyopita kuwa Super
Eagles wataondolewa katika michuano hiyo
iwapo watashindwa kucheza maechi yao.

0 comments:

Post a Comment