Facebook

Sunday 21 September 2014

Clash of the Titans...Chelsea Vs Manchester City

Usithubutu kunywa uji wa mgonjwa...Wala mtoto hatotumwa dukani majira ya saa 12:00 Jion kwa masaa ya Afrika Mashariki mtanange kati ya Vijana wa Darajani,The Blues almaarufu kama Chelsea watakapopambana na The Citizen,Manchester City katika dimba la Etihad katika Jiji la Manchester.

Kwa teknolojia ya sasa ni mambo machache
sana unaweza kuyafahamu bila kutumia
Computer ila kuna mengine yanaeleweka
kabisa kuwa hivi sasa mechi kubwa na yenye
upinzani kisoka ni mechi kati ya Manchester City na
Chelsea.

Kwanza hizi ndizo timu zinazopewa
kipaumbele cha kuchukua ubingwa wa Ligi
kuu ya Uingereza.

Timu hizi zimekamilika kila idara
kuanzia benchi la ufundi, mchezaji mmoja
mmoja na timu kwa ujumla.

Haihitaji Computer kugundua mchezo wa leo
utaamuliwa katikati ya uwanja, hebu fikiria
pale kuna Ramires,Oscar,Willian, Matic na
Fabregas na huku kwingine kuna Yaya Toure ,
Fernadinho, Silva, Samir Nasri kwa kifupi
timu zote zimekamilika katikati ya uwanja.
Uimara wa safu za ushambuliaji wa timu zote mbili pia kunaongeza utamu wa mechi hii Chelsea msimu huu wametibu tatizo lililowatatiza sana msimu uliopita,sehemu ya ushambuliaji,haipingiki Diego Costa amekuwa mwiba kwa beki hivi sasa bali vilevile Manchester City nao si wa kubezwa Sergio "Kun" Aguero,Dzeko na Stephan Jovetic muda wowote ule wanalichungulia goli.

Ukiangalia mechi mbili za mwisho walizokutana ambazo
Chelsea ilishinda zote walikuwa wakitumia
viungo watatu wenye asili ya ukabaji ili
kuwazima Man City wasicheze mpira hapo
David Luiz, Ramires na Matic walifanya kazi ya
kuzia "movement" za kina Nasri, Toure na Silva.
Chelsea ya sasa haina Luiz bali ina Fabregas ni
jukumu la Man City kuwazima kina Fabregas
na Oscar ili waweze kumfanya Diego Costa asipate
mipira , kama Man City
watafanikiwa kwenye hili basi watashinda
mechi ya leo ila wakishindwa basi chelsea
itaendeleza gharika ya ushindi kwa 100%

Imeandaliwa na...
                             Katemi Methsela.

0 comments:

Post a Comment