Facebook

Friday 12 September 2014

Mchakato wa katiba kusitishwa

Kumekuwa na maoni tofauti kufuatia
hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya
maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania.
Katika kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya
Kikwete na Viongozi wa vyama vya siasa nchini
humo wamekubaliana kuwa kura hiyo ya maoni
ambayo ilikuwa ifanyike kabla ya uchaguzi
mkuu mwaka 2015 kinafanyika baada ya
uchaguzi huo
Umoja wa wabunge wa kambi ya upinzani
Tanzania UKAWA hivi karibuni walisusia bunge
la Katiba na kutoka nje kwa kile walichodai
kutekelezwa kwa baadhi ya madai ya msingi.

Deusi Kibamba
Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini
Tanzania anasema hatua za haraka zinapaswa
kuchukuliwa kusitisha vikao vya bunge la katiba
hata kabla ya muda uliopendekezwa wa
Oktobar 4 mwaka huu.
Amesema kuwa iwapo wabunge hao
wataendelea na vikao hivyo wao pamoja na
baadhi ya wananchi wanatarajia kufanya
maandamano hadi mjini Dodoma na kufunga
milango ya ukumbi wa bunge.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii
Robert Mkosamali anasema pamoja na kwamba
fedha nyingi zimekwisha tumika hadi sasa
kinachpaswa kuangaliwa si gharama hizo bali ni
kuangalia ubora wa katiba inayotafutwa hata
kama yaweza kutafutwa kwa muda mrefu na
wka gharama kubwa.
Mkosamali amesema hata nchi zilizopata Katiba
zilichukua muda mrefu na gharama kubwa
akitolea mfano nchi ya Kenya.

0 comments:

Post a Comment