Waendesha mashtaka katika Mahakama ya
Kimataifa ya ICC iliyopo The Hague
wameomba kesi ya Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta kuahirishwa tena. Bwana Kenyatta
anashtakiwa kwa makosa dhidi ya ubinaadam,
lakini upande wa mashtaka umesema hakuna
ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi kwa
sababu serikali ya Kenya inashindwa kutoa
ushirikiano. Mashtaka hayo yanahusiana na
ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007,
ambapo watu zaidi ya 1,200 waliuawa na
karibu watu nusu milioni kkimbia makazi
yao.
Friday, 5 September 2014
KESI YA KENYATTA YAPIGWA KALENDA
Related Posts:
UFARANSA KUUNDA JESHI KUPAMBANA NA MAKUNDI YA JIHAD Ufaransa itaanzisha shughuli mpya za kijeshi katika eneo la Sahel, Afrika Kaskazini, katika juhudi za kuzuia kuibuka kwa makundi ya jihadi. Takriban wanajeshi 3,000 watapelekwa huko, kwa pamoja na wanajeshi kutoka… Read More
Kiwanda cha 'Samsung' chatumikisha watoto Samsung imesitisha uhusiano na kampuni hiyo Kampuni ya bidhaa za elektroniki ya, Samsung imesema kuwa imepata ushahidi wa kuwatumikisha… Read More
Mapigano kati ya Israel na Palestina yazidi kushika kasi Mashambulio ya anga kwenda Gaza na maroketi kwenda Israel yameendelea wakati harakati za Israel dhidi ya wapiganaji wa Palestina zikiingia siku ya saba. Maafisa wa Palestina wanasema watu 172 wameuawa Ga… Read More
Vita kati ya Israel na Palestina vyazidi kupamba moto. Israel na wapiganaji katika Gaza wameendelea kurushiana makombora usiku kucha baada ya Israel kuahidi kuendelea na mashambulizi ili kuzuia maroketi. Wapalestina wapatao 121 wameuawa, kwa mujibu wa vyanzo vya Pal… Read More
Simanzi yatawala baada ya mfanyabiashara maarufu kuawa Mombasa. Watu wawili wenye bunduki wamemuua mfanyabiashara maarufu mjini Mombasa anayeshtakiwa kwa ugaidi nchini Kenya. Mohamed Shahid Butt alikuwa ndani ya gari lake akitokea kwenye uwanja wa ndege siku ya Ijumaa, ambapo… Read More
0 comments:
Post a Comment