Facebook

Friday 12 September 2014

Mwanaume apata dalili za ujauzito Uingereza.

Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza
nchini Birmingham kupata ruhusa ya
kupumzika nyumbani baada ya
kusumbuliwa na homa mithili ya
mwanamke mja mzito.
Amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa
nyakati za asubuhi baada ya mchumba wake
aitwae Charlotte kuwa mjamzito, mtandao wa
Itv news umeeleza.
Habari zinasema mwanaume huyo mwenye
miaka 29 anayefanya kazi ya ulinzi ,amesema
ameongezeka uzito na tumbo limekua mithili
ya aliye mjamzito na kudai kuwa anasumbuliwa
na maumivu ya mgongo na cha ajabu amekuwa
na hamu ya baadhi ya vyakula.
Harry ameripotiwa kuwa na dalili za kuwa mja
mzito miezi miwili baada ya kubaini kuwa
mchumba wake ni mjamzito.
Harry amekuwa akipatiwa dawa na
inasemekana anaweza kudai mafao wakati
akiwa katika mapumziko hayo.

0 comments:

Post a Comment