Facebook

Friday 12 September 2014

Syria yashutumiwa kutumia Gesi ya Chlorine dhidi ya wakazi

Gesi ya Chlorine ilitumika katika
kuwashambulia watu Kaskazini mwa Syria
mwaka huu, hii ni kwa mujibu wa shirika la
kimataifa ambalo linanuia kuweka sheria
zinazoharamisha silaha za kemikali.
Shirika hilo, (OPCW) linasema lina ushahidi
kuonyesha kuwa gesi ya Chlorine ilitumika
katika kuwashambulia wakazi .
Shambulizi lilifanyika mapema mwaka huu,
katika vijiji vilivyo karibu na maeneo ambako
waasi wamekuwa wakipigania na wanajeshi wa
serikali.
Shirika la OPCW limekuwa likijihusisha na
juhudi za kuharibu silaha za kemikali nchini
Syria.
Mwaka mmoja uliopita, Syria ilitangaza
kuharibu silaha za kemikali zilizokuwa
zimewekwa nchini humo kuambatana na sheria
za kimataifa.
Hata hivyo, Syria haikushurutishwa kutangaza
kiwango cha silaha ilizonazo, ambazo
zinaonekana kuwa za kemikali.
Ripoti hii ya hivi karibuni inasma kuwa
kemikali za sumu zilitumiwa kuwashambulia
watu vijijini hasa katika maeneo yaTalmanes, Al
Tamanah na Kafr Zeta Kaskazini ya Syria.
Kadhalika ripoti hiyo inasema kuwa inaamini
kwamba kemikali ya Chlorine ndiyo iliyotumika
katika kuwashambulia wanakijiji.
Inasema wanajua kwamba ni gesi ya Chlorine
iliyotumika kutokana na dalili walizokuwa nazo
wanakijiji , walivyokuwa baada ya matibabu
pamoja na maelezo kuhusu gesi hiyo.

0 comments:

Post a Comment