Facebook

Saturday 6 September 2014

Damu ya waliopona Ebola kutibu Wagojnwa wengine.

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa
damu ya watu ambao wamepona ugonjwa
wa Ebola inaweza kutumiwa kuwatibu
wagonjwa wengine.

Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa
shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa
njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa
wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya
mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza
kukabiliana na virusi hivyo.

Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine
kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja
na chanjo zengine mbili.

Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na
ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili.
Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa
ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado
haijajulikana.

0 comments:

Post a Comment