Facebook

Thursday 25 September 2014

Mwanzilishi wa kampuni ya 'Apple' aliwazuia watoto wake kutumia iPad, iPhone na iPod, fahamu sababu

Bidhaa za kampuni ya Apple zina mashabiki na
wateja wengi duniani, hii inathibitishwa na
foleni kubwa ya watu waliojitokeza kwenye
vituo mbalimbali duniani kununua toleo jipya
la iPhone6.

Tumesikia watu wakiachana ama familia
zikitengana kwa sababu tu baba ameshindwa
kununua bidhaa za kielekroniki za kampuni ya
Apple.

Mwaka jana familia moja nchini China
iliwauza watoto wao ili kupata pesa ya kununua
iPhone5.
Kwa kuzingatia hayo, huenda ukadhani watoto
wa mwanzilishi wa kampuni ya Apple na
mgunduzi wa bidhaa hizo, Steve Jobs wanafaidi
zaidi bidhaa hizo.
Na huenda ukadhani hata kuta za nyumba yao
zingeweza kuwa za mfumo wa simu za kisasa za
kupangusa ‘Screen Touch’ na mawasiliano ya
hali ya juu ndani ya nyumba hiyo kwa mfumo
huo.

Lakini ukweli ni kwamba, marehemu Steve Jobs
hakuwaruhusu hata kidogo watoto wake
kutumia iPhones, iPods wala iPads nyumbani
kwake.
Katika article iliyoandikwa na New York Times
wiki hii, mwandishi wa habari Nick Bilton
ameeleza jinsi ambavyo alishangaa majibu ya
Steve Jobs alipomuuliza jinsi ambavyo watoto
wake wanapenda bidhaa za kampuni hiyo.

“Hawajawahi kutumia kabisa. Tunadhibiti kiasi
ambacho watoto wetu wanatumia teknolojia
nyumbani.” Alijibu Steve Jobs.
Nae mwandishi maalum wa Steve Jobs, Walter
Isaacson ambaye alikuwa akitumia muda
mwingi nyumbani kwa boss wake huyo
alithibitisha kuwa maoengezi ya uso kwa uso
yalitawala katika nyumba hiyo.
“Kila jioni Steve alikuwa akipata chakula cha
usiku na familia yake kwenye meza kubwa
jikoni, wakijadili vitabu na historia na vitu
vingine vingi. Hakuna mtu aliyekuwa na iPad au
computer. Watoto hawakuonekana kuwa
addicted hata kidogo na vifaa hivyo.” Alieleza
Isaacson.

Inaelezwa kuwa hata Steve Jobs hakuwa na
tabia ya kutumia vifaa hivyo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Steve Jobs aliyefariki mwaka 2011
sio mtu maarufu pekee aliyeamini katika
kuweka sheria kali kwa watoto wake kutumia
vifaa hivyo, Chris Anderson, mhariri wa zamani
wa Wired pia alieleza kuwa yeye na mkewe
wamewazuia watoto wao kiasi kwamba watoto
hao huwalalamikia sana wakilinganisha na
uhuru wanaouona katika familia za marafiki zao.
Utafiti uliofanywa katika eneo la Chuo Kikuu
cha California, Los Angeles na kuchapishwa hivi
karibuni unaonesha kuwa siku chache baada ya
kuzuia watoto kutumia vifaa vya kieletroniki
vya simu, ufaulu wa watoto katika masomo
ulipanda ghafla.

Utafiti unaonesha kuwa kwa wastani watoto
nchini Marekani hutumia zaidi ya saa saba na
nusu kwa siku katika matumizi ya simu za
kupangusa na vifaa vingine vya kielekroniki
kama iPads, iPod n.k.

Uamuzi ni wako, kumnunulia mwanao vifaa vya
hivyo au kumuweka mbali na mapinduzi hayo
ya kiteknolojia.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa na stori mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment