Mwanamke
wa Mexicana, Leandra Becerra mwenye umri wa miaka 127 anaetajwa kuwa
mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ameeleza siri ya kuishi miaka mingi
zaidi. Kwa
mujibu wa mjukuu wake mwenye umri wa miaka 45, bibi huyo alimueleza
kuwa siri ya ‘yeye’ kuishi miaka mingi ni kula vizuri, kulala kwa muda
mrefu na kuishi bila kuolewa.
Bi Leandra ambaye alizaliwa August
31, 1887 alikuwa mpiganaji wakati wa mapinduzi ya Mexico mwaka 1910-1919
na alikuwa kiongozi wa kundi la ‘Adelitas’ ambalo lilikuwa linaundwa na
wanawake wanaoenda vitani na waume zao.
Bibi huyo ambaye ana wajukuu wengi huku mjukuu wake mkubwa akiwa na umri wa miaka 73, tayari ameshawazika watoto wake watano. Mjukuu wake aliiambia gazeti la El Hozizonte la Mexico kuwa bibi huyo hivi sasa anatatizo la kubwa la kusikia.
Ameeleza kuwa bibi huyo mara nyingine hulala mfululizo kwa muda wa siku tatu huku akipewa chakula pale anaposhituka. Lakini
akiamka hupenda kula mlo kamili kwa uhakika, kuimba, kutaniana na
kusimulia hadithi mbalimbali zinazohusu maisha na mapambano ya mapinduzi
ya Mexico.
Tofauti na wazee wengi, bi Leandra yeye hana tatizo la sukari hivyo anakula vitu vya sukari na chocolate kadri awezavyo.
ANGALIA PICHA MWANAMAMA MWENYE MATUKIO YA AJABU
Kwa jina
unaweza muita Leilani Franco(Backbend) ana uraia wa nchi mbili
(Uingereza / Philippines) alisafiri katika nafasi umbali wa 20m katika
muda wadk 10.05 katika tamasha la Royal…Read More
Je,wajua kuna waombolezaji wa kulipwa ?
Kila Alhamisi na Ijumaa, shughuli katika mji
wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, huvurugika kwa sababu mamia ya waendesha
pikipiki huzuia barabara kutokana na kukodiwa kuomboleza msiba kwa
malipo.
Kelele za saut…Read More
Harusi ya Nyani yatia Fora India
Zaidi ya wakazi 200 katika kijiji kimoja kaskazini mwa India wamehudhuria sherehe ya harusi ya nyani wawili. Harusi hiyo iliandaliwa na mmiliki wa nyani hao, ambaye alisema nyani dume ni kama "mwanaye".
Sherehe hiyo ilif…Read More
MTOTO AMUOA MAMA YAKE WA KAMBO
Bwana mmoja nchini Ufaransa amemuoa mke wa zamani wa baba yake (mama
yake wa kambo) baada ya kushinda kesi iliyodumu kwa miezi kadhaa.
Harusi ya Eric Holder, 45, na aliyekuwa mama yake wa kambo Elisabeth
Lorentz, 48, i…Read More
0 comments:
Post a Comment