Waziri mkuu wa Misri, Hazem el-Beblawi na baraza lake la mawaziri wamejiuzulu.
Katika taarifa ya moja kwa moja kupitia
televisheni, Bwana El-Beblawi alisema kuwa Misri imeshuhudia ongezeko la
migomo katika sekta ya umma katika wiki chache zilizopita.Serikali hiyo ya mpito ilianza kazi mwezi Julai mwaka jana baada ya jeshi kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Mosri
Taarifa zinasema kuwa uamuzi wa baraza la mawaziri kujiuulu ulitokea baada ya mkutano kati ya mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi.
Inaarifiwa kuwa al-Sisi anatarajiwa kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake ili kugombea Urais.
0 comments:
Post a Comment