Facebook

Tuesday, 27 May 2014

Hiii hapa sababu iliyomfanya kaka wa damu wa Kim Kardashian kutohudhuria harusi ya dada yake.


Rob Kardashian
Unaweza usiamini lakini ukweli ndio huo mtu wangu, Unaambiwa kaka wa damu wa mwanadada Kim Kardashian hajahudhuria harusi ya dada yake kwa madai ya kuchoshwa na jinsi dada yake huyo pamoja na mumewe Kanye West wanavyofanya vurugu nyingi za maonyesho ya mali na nguo.
Siku hiyo ya harusi kaka huyo wa Kim, Rob Kardashian, alionekana katika Uwanja wa ndege wa Los Angeles alikosafiri na mama yake muda ambao Kim na Kanye walikuwa wakifunga ndoa mjini Florence Italia.
Robkardashian3
Taarifa nyingine zinadai kuwa Kim pia alikasirishwa na kitendo cha kaka yake huyo kushindwa kupunguza unene alionao kutokana na kwamba angetokea vibaya kwenye picha za familia.
Rob Kardashian2
Rob hakuacha kuhudhuria harusi hiyo peke yake bali pia aliacha kushiriki kila kitu kilichoandaliwa na familia yake ikiwa ni pamoja na ile Pre Wedding Party, Alipoulizwa kwanini hakushiriki harusi ya dada yake Rob hakujibu chochote. Mtoto huyo pekee wa kiume katika familia ya Kardashian hajaonekana hadharani tangu January mwaka 2014 baada ya kuamua kukaa mbali na macho ya watu kutokana na kuongezeka unene wa kupindukia.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali zinazowahusu mastaa

0 comments:

Post a Comment