Facebook

Wednesday, 3 September 2014

Rais Obama alaani mauaji ya mwandishi


Mwandishi Mmarekani Steven Sotloff aliyeuawa kwa kunyongwa na wapiganaji wa kiisilamu
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Marekani haitatishwa na mauaji wa mwandishi mwingine wa habari Mmarekani na kundi la Islamic state.
Akiongea na waandishi wa habari nchini Astonia Rais obama amesema kuwa mauaji hayo yanaichochea Marekani kukabiliana ziani na magaidi
Mapema Marekani ilisema kuwa kanda ya video inayoonyesha kuchinjwa kwa mwandishi huyo Steven Sotloff ni ya ukweli
Video hiyo iliyotolewa na kundi la wanamgambo wa Islamic State inamuonyesha mwanamme aliyejifunika uso wake na kisu mkononi akisimama juu ya Sotlof.
Nchini uingereza waziri mkuu David Cameron ameongoza mkutano wa kamati ya dharura ya serikali kujalidili jinsi itakavyojibu tishio la kutaka kumuua mateka raia wa uingereza.
Kwenye video hiyo mwanamgambo aliyejifunika uso na anayezungumza kiingereza anayaonya mataifa ya kigeni na kuyataka kusitisha harakati zao dhidi ya kundi la Islamic State.
Sotlof ni mwandishi wa pili wa Mmarekani kuuawa kwa kukatwa kichwa ndani ya mwezi mmoja baada ya mwandishi mwingine James Foly kuuawa kwa kukatwa kichwa mwezi uliopota na wanamgambo wa ISIS.

Related Posts:

  • Viongozi wa Upinzani wavalia sare za wanafunzi KenyaBaadhi ya viongozi wa upinzani nchini Kenya wamevalia mavazi yanayofanana na sare za wanafunzi wakiitaka serikali kulipa walimu nyongeza ya mishahara. Walimu wamekuwa mgomoni tangu kufunguliwa kwa muhula wa tatu na Serikali i… Read More
  • Wanasayansi watengeneza figo maabara. Je una matatizo ya figo ? Ikiwa jibu lako ni ndiyo kuwa na subira, maanake hivi karibuni figo zilizoundwa kwenye viwanda na maabara vitakuwepo kuwasaidia. Nafahamu kuwa waganga wengi wamewaahidi tiba lakini hii sio hekaya tu… Read More
  • Bomu laua watu 6 katika makao ya Rais Somalia.Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka karibu na lango kuu la jumba la rais katika mji mkuu wa Mogadishu. Takriban watu sita wamefariki,ikiwemo walinzi wa rais.Raia mmoja wa Uturuki pia aliuawa. Wengine 10 waliripotiwa kuj… Read More
  • Papa awasili Marekani apokewa na ObamaKiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani katika siku ya kwanza ya ziara ya kihistoria nchini humo ambapo amelakiwa na Rais wa nchi hiyo Barack Obama. Papa Francis aliwasili kwenye uwanja wa n… Read More
  • Panya wasababisha kifo 'Jela ya Mandela'Watu karibu 4,000 wameondolewa kutoka jela ya Pollsmoor nchini Afrika Kusini baada ya panya wengi kuvamia gereza hilo na kusababisha kifo cha mfungwa mmoja. Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela aliwahi kufungwa kati… Read More

0 comments:

Post a Comment