Facebook

Monday, 1 September 2014

Tetesi za Usajili Barani Ulaya na BantuTz SPORTS

BantuTz SPORTS
Taarifa zilizo ingia hivi punde.

Klabu ya QPR wanakaribia kumsajili kiungo mkabaji kutoka klabu ya Tottenham,Sandro ambaye anaonekana kukosa nafasi katika kikosi cha Mauricio
Pochettino.QPR vilevile wako katika makubaliano na winga machachari Aaron Lenon kutoka klabu hiyo.

Hatimaye kiungo Hotlby amewasili Hamburg tayari kwa vipimo vya afya kutoka Spurs kwa mkopo wa muda mrefu.

Manchester United wapo tayari kuwaachia
wachezaji wake makinda Tom Lawrence na
Nick powell kujiunga na klabu ya Leceister
City kwa mkopo,huku Tom Lawrence anaweza
jiunga moja kwa moja (SkysportNews)

West Ham na QPR zinapigana vikumbo kuwania saini ya mshambuliaji hatari Jermain Defoe aliyojiung Toronto FC ya Marekani,Redknapp anaongoza mbio za kuungana na Mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa nae akizifundisha Tottenham,Porthmouth na West Ham.

Manchester United wametuma ofa ya
kutaka kumsajili kiungo wa Southampton
Morgan Schneiderlin.

Kiungo wa Chelsea Mark Van Ginkel amejiunga rasmi na AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu,AC Milan wamethibitisha hilo kupitia ukurasa wao wa twitter.

Manchester United wamefanya mawasiliano
na wakala George Mendez kwa ajili ya kutaka
kumnasa kiungo Joao Moutinho
(Goal.com)

West Ham wamemsajili Winga machachari kutoka Marseille ya Ufaransa Morgan Amalfitano,ambaye yuko Uingereza hivi sasa akifanyiwa vipimo vya afya

Manchestet United wamekubali ofa toka
QPR kwa ajili ya kuwapa kinda Will kean kwa
mkopo wa mwaka mmoja.

Andre Ayew amekataa ofa kutoka QPR,West Ham na Swansea huku akipendezwa zaidi kujiunga kati ya Arsenal au Spurs.

Dany Welbeck yupo karibu kujiunga na
Tottenhan Hotspurs kwa mkopo wa muda mrefu.

Hivi Punde,AC Milan wametangaza kumsajili winga kutoka Palermo ya Italia Jonathan Biabiany,26 ambaye amesaini mkataba wa miaka 4.

Hatem Ben Arfa anakaribia kujiunga na klabu ya Lyon ya Ufaransa baada ya kukataa kwenda Birmingham kwa mkopo huku klabu yake ya Newcastle ikiwa haina mipango na mchezaji huyo msimu huu.

Taarifa zinasema huwenda cleverley
akajiunga na Evarton mapema leo.Baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Aston Villa

Winga machachari wa Mabingwa Man City,Scot Sinclair yuko mbioni kujiunga na Stoke City baada ya kufunguliwa milango ya kuondoka.

Kwa taarifa zaidi endelea  tembelea www.bantutz.com

~Katemi Methsela.

Related Posts:

  • Gerardo Martino ajiuzulu Barcelona !!   Gerardo Martino ataacha kazi ya Ukocha wa Barcelona mara baada ya Jana kupokonywa Ubingwa wa La Liga baada kutoka Sare 1-1 na Atletico Madrid ambao wameutwaa Ubingwa huo na kuiacha Barca ikitoka mik… Read More
  • Man Utd yamsaini kipa kinda kutoka Serbia   MANCHESTER UNITED imekubaliana na Klabu ya Serbia, FK Vojovdina, ili kumsaini Kipa wao Chipukizi Vanja Milinkovic. Milinkovic, Miaka 17, aling’ara mno akiidakia Serbia Mashindano ya Vijana ya… Read More
  • Paundi million 70 kumng'oa Luis Suarez Liverpool   Real Madrid wametenga paundi milion 70 ili kumnasa straika wa Liverpool na mfungaji bora wa Ligu kuu England msimu huu Luis Suarez. Real Madrid pia wanajipanga kumwachia Karim Benzema anayewaniwa na Arsenal n… Read More
  • Park Ji Sung atangaza kustaafu soka....   Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Man united na timu ya taifa ya Korea Park Ji Sung amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 33 na hii inatokana na majeruhi ya mara kwa mara ya goti yanayomwandama. Park aliyeiche… Read More
  • Ngebe,Vitimbi, Vituko vyatawala Uchaguzi mkuu Simba Vitimbi, vituko, na kejeli zilitawala jana makao makuu ya klabu ya Simba wakati wagombea uongozi wakirudisha fomu, huku mgombea urais, Michael Wambura akiambatana na viongozi wa dini waliomwaga sala. Wambura, ambaye … Read More

0 comments:

Post a Comment