Mshambuliaji wa Galatasaray Didier Drogba amefanya kitendo ambacho kimezidi kumpa sifa kubwa pindi linapokuja suala la kurudisha kwa jamii.
Drogba na wachezaji wenzie wa Galatasary walivaa ‘helmets’ kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuonyesha sapoti juu ya tukio lilotokea machimboni, lakini muivory coast akachukua hatua nyingine ya ziada kuwasaidia wahanga wa maafa akiwa kama balozi wa Umoja wa Mataifa.
“Mimi ni balozi wa U.N na nitafanya kila kitu kusaidia watu waliopata maafa kule Soma,” Drogba aliwaambia waandishi wa habari.
“Lakini sihitaji mtu yoyote atumie jina langu kujipatia umaarufu kupitia janga hili, mimi sio mtu wa kujipromoti kwenye vitu kama hivi.”
Tarehe 13 mwezi huu kwenye migodi ya makaa kulitokea mlipuko mkubwa uliosababisha vifo vya watu 301.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali za michezo kwa wakati muafaka
0 comments:
Post a Comment