Facebook

Friday, 16 May 2014

Birthday ya mwigizaji Vicenti Kigosi ray, Johari ampa salamu tata, isome hapa

Leo ni birthday ya mwigizaji Vicenti Kigosi ray, Johari ampa salamu tata, isome hapa
Leo mwigizaji maarufu nchini Vicent kigosi - Ray anasherehehea siku yake ya kuzaliwa huku akipata salamu mbalimbali za pongezi toka kwa mastaa mbalimbali nchini.
Moja ya watu wa kwanza kwanza kumpa salamu hiyo ni swahiba na rafiki yake mkubwa, JB akifuatiwa na mpenzi wake wa zamani Johari ambaye salamu yake inadaiwa na wachunguzi wa mambo kuwa ni kwa namna flani inamponda mpenzi wa sasa wa Ray , Chuchu hans, kutokana na maneno yaliyotumika ya salamu hiyo ambayo Johari anadaiwa kuwahi kuyatumia kumponda Chuchu siku za nyuma.

JB ameandika
''Happy birth day mdogo wangu ray.mungu akupe haja ya moyo wako.''

Na huku Johari akiandika 
''Happy birthday director wa rj na swaiba wangu mungu akuongoze akupe maisha marefu na akuepushe na ‘’mabarazuri’’
Hongera sana kaka kigosi. Mungu akupe maisha marefu

0 comments:

Post a Comment