
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaanza ziara ya siku 26 katika
Mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara kukagua uhai wa chama na
maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu.
Hata hivyo, duru za kisiasa zinaonyesha kuwa ziara hiyo ni sehemu ya
kuushambulia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao walitoka bungeni
wakati wakijadili mchakato wa Katiba Mpya wakidai kutoridhishwa na
mwenendo wa Bunge hilo. Ukawa pamoja na CCM walikwishafanya hivyo
Zanzibar.
Wakati Kinana akifanya ziara katika mikoa hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wazazi wa CCM, Abdallah Bulembo amekwishaanza kushambulia Mikoa ya
Kusini, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye alisema
Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ataanza ziara yake Mkoa
wa Tabora, ambako atatembelea wilaya zote kuanzia Mei 8 hadi 18. Mkutano
wa kwanza utaanza leo katika Wilaya ya Igunga.
Baadaye ataendelea Mkoa wa Singida kuanzia Mei 19 hadi 26 na kumalizia
Mkoa wa Manyara, ambako ataanza Mei 26 hadi Juni 3 mwaka huu.
Nape alisema pia kuwa wamemkabidhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ripoti ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi
ili afahamu changamoto za mikoa hiyo.
0 comments:
Post a Comment