Facebook

Monday, 12 May 2014

Chris Brown aongezewa siku za kukaa jela....


Uhuru wa Chris Brown kwa sasa bado ni ndoto sababu Ijumaa iliyopita (May 9) jaji wa mahakama ya Los Angeles alimhukumu mwimbaji huyo kifungo cha mwaka mmoja jela (siku 365), baada ya kukiri kuvunja masharti ya kesi yake ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna mwaka 2009.

Jaji anayeisikiliza kesi hiyo, James R. Brandlin alimuondolea siku 234 za kifungo hicho ambazo tayari amezitumikia kwa kukaa rehab na jela, hivyo anatakiwa kumalizia siku 131 zilizobaki.

Breezy aliwekwa jela toka katikati ya March baada ya kuvunja sheria za rehab huko Malibu, alipoamriwa kukaa kwaajili ya matibabu ya kukabiliana na hasira.

Kesi zinazomkabili mwimbaji huyo wa R&B kwa kiasi flani zimeathiri muziki wake japo management yake inajitahidi kuendelea kutoa nyimbo mpya akiwa jela. Mwezi March aliachia video ya version ya tatu ya wimbo wake ‘Loyal’ aliyowashirikisha Lil Wayne na Tyga, na mwezi uliofuata (April 15) aliachia video ya moja ya nyimbo zitakazokuwepo katika album yake ya ‘X’, “Don’t Be Gone Too Long” aliomshirikisha Ariana Grande.

Mwezi February mwaka huu Brown alitangaza tarehe mpya ya album yake kutoka (May 5) ambayo imemkuta jela. Album hiyo imeahirishwa mara kwa mara toka mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua hatma ya Chris Brown katika kesi hiyo

0 comments:

Post a Comment