Wakala wa kiungo wa Machester City Yaya Toure amekashifu kupuuzwa kwa kiungo huyo kutoka Ivory Coast.
Dimitri Seluk alikashifu ujumbe wa kheri njema
kwa Toure ambaye alikuwa anaadhimisha siku kuu ya kutimiza miaka 31
mnamo mei tarehe 13.Dmitri Seluk
"'Itakuwaje siku ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Roberto Carlos rais wa Anzhi alimnunulia gari aina ya Bugatti na eti bwenyenye mwenye Man city anatuma keki na ujumbe wa tweeter? Nilitarajia watamtambua hata kwa salamu tu lakini Iwapo hawatamheshimu basi huenda akaondoka Etihad "
Toure aliandikisha kandarasi mpya ya miaka minne mwaka uliopita licha ya Seluk ambaye amemuakilisha Toure kwa zaidi ya miaka kumi kutishia kuwa kiungo huyo wa Ivory Coast angehama Etihad.
Uhusiano baina ya mchezaji huyo bora barani Afrika na Seluk umedumu kwa miaka mingi kiasi ya kuwa Toure alimpa mwanawe wa pili jina la Seluk.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua hatma ya Yaya Toure ndani ya Man City
0 comments:
Post a Comment